Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa maonesho/michezo ya kuigiza na filamu basi pengine eneo maarufu ambalo linaoneshwa kupitia Apple TV la SILO pengine utakua unalijua
Unesho hili linafikikia ukingoni kwa upande wa toleo la kwanza na Apple TV wameona kwamba watoe sehemu ya kwanza tuu katika mtandao wa Twitter.
Kwa makampuni makubwa hivi huwa hawafanyagi vitu kama hivi bila kuwa na sababu ya msingi ambayo itakua na manufaa hata kwao.
unaweza kuta wamefanya hivi makusudi ili kuwavutia watu waweze kujiunga kwa wingi na huduma yao ya kulipia ya Apple Tv
Kama utaangalia sehemu hiyo ya kwanza na kuipenda itakuladhimu kulipia huduma hiyo ili kuangalia sehemu zingine zilizobakia.
Kwa mimi nalifuatilia onesho hili, na kwa haraka haraka mimi limenivutia? Na wewe unataka kutazama sehemu hiyo ya kwanza? Mchawi bando tuu maana unaweza kuitazama hapa chini
3 days until the #Silo finale.
Here’s the entire first episode. pic.twitter.com/lIcTXCQ9D6
— Apple TV (@AppleTV) June 27, 2023
kingine ni kwamba isifikiriwe kabisa kwamba Apple watakua wanaonesha bure bure maonesho yake yanayopatikana katika huduma yake ya kulipia.
Hii ni wazi ni kuvuta wateja wapya, kujiunga na huduma…
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo katika eneo la comment, je ulishawahi kuangalia onesho hilo au ndio mara yako ya kwanza? Je umelipokea vipi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.