Apple ni moja kati ya makampuni makubwa ya teknolojia ambayo mara kwa mara yamekua yakipenda kujitofautisha sana na makampuni mengine kabisa.
Ni mara chache sana Apple wanakua wafanana katika bisahaa na makampuni mengine na mara nyingi ikitokea hivyo basi wenyewe huwa ndio wanakua wabunifu wa kwanza.

Tuliandika >>HAPA<< kuhusiana na Apple na USB Type-C
Kwa mara ya kwnza aina hizi za USB zitaanza kupatikana katika iPhone 15 na iPhone 15 Pro/Ultra na zitakua na muonekano wa Type-C.
Hapa kinachofanyika ni kwamba chaja za Android hazitaweza kuchaji iPhone hizo na hata kama ikitokea zimeweza basi hazitachaji kwa spidi ambayo chaji (USB Type-C) kutoka Apple ingefanya.
Ili kuwezesha hili kampuni itakuja na sakiti ya IC (Integrated Circuit) ambayo ndani yake itakua na teknolojia mpya ya MFi-Certified
Kazi yake kubwa ni kutofautisha vifaa vya USB Type-C na Type-C ile ambayo itakua ni chaji kutoka Apple –ambayo imetengenezwa mahususi kwa vifaa vya kampuni hiyo tuu.
Kingine ni kwamba kama chaji hizi zitatoka basi watumiaji wa vifaa vya kampuni hiyo itabidi wahakikishe wanatumia chaji Orijino kutoka kwao.
Mpaka sasa bado haiku wazi katika swala zima la athari, je itaathiri uhamishaji wa taarifa (data) kwa haraka kutumia waya huo? Vipi kuhusu kuingiza chaji kwa haraka zaidi (fast charging)?
Soma ziadi kuhusiana na USB >>HAPA<<
kampuni bado haijapoa kabisa licha ya kuja na hili la kujitofautisha ni bado watazidi kufanya mengi zaidi ambayo yataihakikishia kampuni kuzidi kuwa juu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa Apple wanachofanya katika kuhakikisha kwamba wanazidi kujitofautisha na watu wengine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.