Fikiria uwezo wa kutumia kamera ya iPhone iwe kama webcam kwa watumiaji wa mac, Hili linakuja hivi karibuni.
Kwa sasa Mac ina program endeshaji inayojulikana kama MacOS Ventura na toleo lake jipya linasemekana kuwa na uwezo huu wa kuruhusu kutumia kamera ya iPhone kama webcam.
Hii ni kwamba kwa watumiaji wa iPhone na Mac wakiweza kufanya hivyo ni kwamba wanaweza kurahisiha baadhi ya mambo hata kuyaboresha pia.
Fikiria huduma za simu za kivideo kama vile Facetime, Zoom na nyingine nyingi, kwa kutumia teknolojia hii zitaweza kufanyika kwa ufanishisi Zaidi katika eneo la kamera.
Hapa kinachofanyika ni kwamba kunakua na kifaa maalum ambacho kitakua kinaishikialia simu kwenye laptop ya Mac (kwa juu).
Apple will let you use your iPhone as a webcam with continuity #WWDC22 pic.twitter.com/pzGzfdcm06
— The Verge (@verge) June 6, 2022
Kingine kizuri ni kwamba kwa asilimia kubwa kampuni ya Apple imesema kuwa hutahitaji vifaa vipya zaidi (japokuwa hatuna uhakika kama vya zamani vyote vitaweza) cha kufanya ni kuhakikisha kifaa chako kina toleo la juu kabisa la program endeshi (Operating system).
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, hili umelipokeaje? Je unahisi makampuni mengine watafuata nyendo hizi za Apple.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.