Kumbuka iPod ya kwanza kabisa iliingia sokoni mwaka 2001 na ikabadilisha kabisa jinsi watu wanavyosikiliza na mapenzi ya muziki yaliongezeka kwa kiasi kikubwa.
iPod ni mojawapo ya kifaa cha kielektroniki ambacho kimeisaidia sana kampuni ya Apple na imekua ni moja katika ya bidhaa ambayo imeliokoa kampuni –maana ilikua bado kidogo lifilisike — mpaka leo ni kampuni tajiri kabisa duniani.

Kampuni imeweka wazi kwa uma kuwa imeacha kuzalisha bidhaa hizo jumanne hii, kumbuka ile ya kwanza kabisa ilizalishwa 2001 kama nilivyosema.
Lakini ile ya mfumo wa ku’Touch ilizinduliwa 2007 (ndio! ilitoka mwaka mmoja na iPhone ya kwanza kabisa). Sasa Mfumo Huu wa iPod kwakua bado iko katika baadhi ya maduka ya Apple….
….inabidi waache kuzalisha kabisa, lakini vile vile wauze zile iPod ambazo zipo kwenye maduka yao mopka ziishe kabisa (huwezi jua, pengine wanaweza wakauza bei ya punguzo).

Apple imezalisha matoleo mengi sana ya iPod lakini bidhaa yao kubwa ambayo iliua soko la bidhaa hiyo ni iPhone. Kumbuka kwa mwaka 2014 napo waliacha kutengeneza ile iPod maarufu sana ya zamani yenye duara kati linalobonyezeka na ka kioo kadogo.
Haikuishia hapo 2017 napo wakaacha kabisa uzalishaji wa iPod Nano na iPod Shuffle ….pengine hizi zilikua ni ishara kuwa jambo hili linakuja!
Niandikie Hapo Chini Katika Uwanja Wa Comment, Ushawahi Kutumia iPod Ipi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.