Arm na Apple waliingia katika makubaliano ya kutengeneza chip kwa ajili ya vifaa vya Apple na chip hizo ni zile zinazojilikana kama Silicon Chip.
Kwa Sasa Apple wameongeza mkataba (wa muda mrefu) kutoka katika kampuni hiyo ya Arm ambayo inamilikiwa na kampuni mama ya Softbank.
Ni wazi kwamba dili hili litkaua ni la muda mrefu Zaidi maana kwa taarifa za harakaharaka tuu ni kwamba mkataba huu utafikia mpaka 2040.
Kwa sasa ni wazi kwamba chip za Arm zipo katika kila kifaa cha Apple kuanzia katika Apple Watch, iPad na hata iPhone na hili lilibadilika kuanzia mwaka 2020.
Kutokana na umaridadi wa kampuni ya Arm Apple imeweza kutengeneza vifaa vyenye ufanisi wa hali ya juu –Chip hizi zimeleta mapinduzi kwa Apple.
Wengine wanasema kwamba ubia wa Apple na kampuni hiyo haujaanza sasa hivi kwa maana ya kwamba hata katika kompyuta ya Apple Newton ilikua inatumia Chip kutoka katika kampuni hiyo.
Kingine ni kwamba kampuni hiyo ya Arm imeamua kujiweka katika soko la hisa na kuvutia wawekezaji kutoka nje huku makampuni kama vile Nvidia, Google, na Samsung wao wamewekeza tayari.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment je ni sawa kwa Apple kungia mkataba mwingine wa muda mrefu na Arm?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.