Kwa kipindi kirefu makampuni mbalimbali hasa ya nchini Uchina yamekuwa yakitengeneza makava ya simu hasa za iPhone yanayokuwa na betri ndani yake. Makava haya yamekuwa yakisaidia kuchaji simu pale yanapokuwa yamevalishwa kwenye simu na hivyo kuongeza muda utakaoweza kutumia simu bila kuchaji.
Na sasa kampuni ya Apple imeamua kuingia katika biashara hiyo, imetengeneza rasmi makava ya iPhone 6s yanayokuja na betri la chaji ya kutosha.
Kava ilo litafanya kazi kwenye simu ya iPhone 6 na iPhone 6s ingiwa limetengenezwa likilenga zaidi watumiaji wa iPhone 6s
Ingawa hajataja kiwango cha uwezo wa chaji za betri zilizohusika katika makava hayo kampuni hiyo imesema utumiaji wa kava ya iPhone 6s inatakiwa ikupe kati ya masaa 18 hadi 25 ya chaji zaidi – ukilinganisha na bila kutumia. – Haya ni masaa mengi sana!
Kutokana na Apple wenyewe kuwa ndio wamiliki wa programu endeshaji ya iOS ya kwenye simu za iPhone basi wameweza kufanya mengi katika kuunganisha simu na mfumo wa betri hilo la kwenye kava. Mfano kupitia eneo la ‘Notification’ katika simu yako ya iPhone 6s utaweza kuona hadi kiwango cha chaji kilichobaki kwenye betri la kwenye kava. Ukitumia makava ya betri ya makampuni mengine hutaona kitu hichi.
Pia wakati makava yenye betri kutoka makampuni mengine yanaitaji mfumo wa waya za kuchajia wa USB ndogo, kava hili kutoka Apple litatumia waya kama wa kuchajia simu hiyo kwa ajili ya kuichaji pia. Hii inamaanisha utumiaji wa kava ili utapunguza mzigo wa kubeba chaja kwa mtumiaji.
Ukitazama vizuri utaona kuna kinundu kidogo, kinundu hicho ndicho eneo lenye betri kwa ndani yake. Ata ukivalisha kava ilo bado utaweza kutumia sehemu zengine zote muhimu za simu yako kama vile kuongeza sauti, eneo la kuchomeka ‘earphone’ n.k.
Bei?
Kava ilo linapatikana kwa dola 99 za kimarekani, hii ni takribani laki 2 na ushee za bongo. Uwepo ma maduka mbalimbali ya vifaa rasmi vya Apple nchini unaleta uhakika wa wewe kuweza kupata kava hizi mapema tuu.
No Comment! Be the first one.