App ya Books toka kwa kampuni ya Apple ni maarufu sana ambayo inawawezesha watumiaji kupata vitabu vile na vya bure na hata vile vya kulipia, lakini ni wazi kama unatumia kifaa cha Apple ambacho kina kioo kidoggo pengine umekutana na shida katika kusoma machapisho hayo.
Ukaichana na hayo tuu kama una kitabua ambacho kina kurasa nyingi kukisomea katika kifaa hicho kila siku kidogo inaweza ikaleta ukakasi sio?
Pengine hii ni moja ya sababu ambayo kampuni imeiona mpka imeamua kuja na teknolojia ambayo itakua na uwezo wa kukusomea maneno katika kitabu husika huku wewe ukiwa unasikiliza tuu.
Basi kwa taarifa yako ni kwamba kipengele hiki ilibidi kitokea kuanzia mwaka jana mwishoni lakini kingine ni kwamba hii ni tofauti kabisa na zile Audiobook kinachofanyika hapa ni kwamba kunakua na roboti ambalo linakusomea maandiko ya kitabu hiko.
Kwa haraka haraka unaweza ukasema kuwa teknolojia hii (AI) haina tofauti kubwa na ile ambayo inatumika katika Siri.
Kingine cha kutilia maanani ni kwamba waandaji wa vitabu husika wakiwa wanavipandisha vitabu vyao katika soko watakua na uwezo wa kuruhusu teknolojia hii kufanya kazi katika vitabu vyao.
Hapo wateweza chagu hata baadhi ya sauti — ambazo zipo chache — kama sauti za kusikika zikisoma vitabu hivyo kwa watumiaji wa vitabu hivyo.
Mara kwa mara Apple imekua moja kati ya kampuni ambazo zipo mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inawaletea wateja wake huduma na bidhaa bora na hii ni kwa njia ya maboresho, masasisho na kuwaletea huduma na vifaa vipya kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je ushawahi kutumia App hii ya Books kutoka Apple, je unahisi huduma hii mpya itasaidia sana watu kusoma vitabu vingi zaidi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.