Apple wameleta sasisho jipya (update) kwa programu endeshaji yao ya iOS 8, toleo hilo jipya linalotambulika kama iOS 8.3 litakubali kwa iPhone, iPad na IPod touch zote zinazotumia toleo la iOS 8 na linaleta maboresho kadhaa na pamoja na Emoji mpya na za kuvutia zaidi.
Katika toleo hili wamefanya maboresho katika eneo la uchaguzi wa emoji hii ikiwa ni pamoja na kuwapa watumiaji uwezo wa kuchagua aina mbalimbali za emoji mpya zilizoingizwa kwenye mfumo huo wa kimataifa wa Emoji.
Emoji ni ‘vikatuni’ ambavyo huwa vinatumika katika app mbalimbali za kuchati kama vile WhatsApp, Facebook, Viber na siku hizi ata kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter n.k

Kama tayari ulishaanza kuona kifaa chako kinapata matatizo kwenye eneo la WiFi, Bluetooth labda na ata kwenye utumiaji wa kibodi mpya kutoka kwenye soko la apps basi hilo nalo limerekebishwa katika toleo hili jipya. Pia kwa watu wanaotumia akaunti ya Google pia yamefanywa maboresho ya kurahisisha kuunganisha akaunti yako ya Google na kifaa chako.
iOS 9 itakuja lini??
Habari zilizoenea na za kuaminika ni kwamba toleo jipya la iOS 9 linaweza kutambulishwa ifikapo mwezi wa sita. Je kutakuwa na chochote kipya? Endelea kutembelea TeknoKona.com na utakuwa wa kwanza kufahamu!
No Comment! Be the first one.