Leo kampuni mashuhuri kwa utofauti na mfumo wa kipekee wa kuingiza sokoni matoleo ya simu na tableti zake siku ya leo wametambulisha simu mpya ya iPhone 6 inayokuja na matoleo mawili ya kitofauti – iPhone 6 na iPhone 6 Plus. Pia Apple wametambulisha saa janja itakayokuwa inafahamika kama Apple Watch, kitu cha tatu ni mfumo mpya wa malipo ambao mtumiaji wa iPhone ataweza kulipia huduma au bidhaa kutumia simu yake yenye akaunti ya Apple ID iliyounganishwa na akaunti ya benki (Visa, MasterCard). Fahamu haya yote hapa.
iPhone 6 na iPhone 6 Plus
Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni pamoja na kukuza ukubwa wa simu za iPhone. iPhone 5 ilikuwa na kioo cha ukubwa wa inchi 4 (iPhone 4 ilikuwa na kioo cha inchi 3.5), iPhone 6 inakuja na kioo cha ukubwa wa inchi 4.7 na iPhone 6 Plus kioo cha ukubwa wa inchi 5.5. Haya ni mabadiliko makubwa kwani Apple huko zamani walikuwa wakiongea dhidi ya simu zenye vioo vikubwa lakini hivi karibuni wameshuhudia simu za Android zenye vioo vikubwa zikifanya vizuri sokoni mfano wa Samsung Galaxy na zinginezo. Tazama kwa ufupi sifa za simu hizi;
Sifa za iPhone 6
- Kioo – Inchi 4.7 / 1334 X 750 Pixels / Retina HD
- Diski Uhifadhi – GB 16, GB 64 na GB 128
- Programu Uendeshaji – iOS 8
- Simu ni ya alumini (Aluminium Cover)
Sifa za iPhone 6Plus
- Kioo – Inchi 5.5 / 1920 X 1080 Pixels /Retina HD
- Diski Uhifadhi – GB 16, GB 64 na GB 128
- Programu Uendeshaji – iOS 8
- Simu ni ya alumini (Aluminium Cover)
- Zote zitapatikana katika rangi ya dhahabu, kijivu au shaba (silver)
Sifa za Ujumla
64-bit A8 chip: Apple wamejitaidi katika kuzifanya iPhone 6 kuwa kati ya simu za mwanzo zenye uwezo mkubwa kiufanisi kwa kutumia teknolojia ya 64bit na chip zenye nguvu A8. Pamoja na hii zimewekwa pia M8 ‘co-processor’ zenye kusaidiana na chip za A8 katika kuhakikisha simu zinakuwa katika ufanisi wa hali ya juu bila kutumia chaji nyingi na hivyo kuongeza muda wa betri kukaa na chaji.
Kamera ya 8 – Megapixel: Kamera nayo imeboreshwa kwa kuongezwa uwezo wa kuboresha muonekano bila ya mtumiaji kuhusika (sensors), hii ikiwa ni pamoja kuboresha picha kutokana na hali ya mwanga au rangi pale picha inapopigwa.
Intaneti ya kasi zaidi? -LTE! – Tatizo ni tulipo, ila simu za iPhone 6 kupitia teknolojia ya LTE zinaruhusu hadi intaneti ya kasi ya MB 150 kwa sekunde ikilinganishwa na iPhone 5 na zinginezo zilizo na uwezo wa MB 100 kwa sekunde.
Betri yenye uwezo zaidi: Apple wamedai ya kwamba batri za iPhone 6 na 6PLus zinakuwa na uwezo mkubwa zaidi kulinganisha na za iPhone 5. Hapa hatutaki kwenda kwa undani sana…
Teknolojia ya QuickType kwenye ‘keyboard’ na uwezo wa kutumia ‘keyboard’ mpya. Kupitia iOS 8 keyboard itakuwa inarekodi na kutabiri maneno kwa jinsi unavyoitumia, na pia Apple wataruhusu watengenezaji wengine wa Apps kuweza kubuni na kutengeneza Apps za keyboard zinazoweza kutumia kama mbadala wa keyboard za iOS 8.
MFUMO WA MALIPO
Kwa kutumia teknolojia inayofahamika kama NFC (Near-field communications) watumiaji wa iPhone 6 wataweza kufanya malipo mbalimbali ya bidhaa au huduma kwenye sehemu zinazotumia kifaa chenye kuweza kuwasiliana na simu zenye NFC. Hii ni juhudi ya Apple kuingia katika ushindani mkali na makampuni kama Amazoni na Paypal.
APPLE WATCH
Kumiliki saa janja hii itakugharimu takribani Tsh Laki 6 ($350)…upo hapo? Na kuweza kuitumia inakuitaji uwe unamiliki iPhone 5 au 6, kwani ni kupitia simu hizi ndio utaweza kufanya nayo mawasiliano. Pia kupitia ushirikiano na kampuni zingine Apple imewezesha saa hizi kukuonesha vitu kama ‘status’ za Facebook , matokeo ya michezo au kukuonesha wapi umepaki gari lenye mfumo wa iOS kama BMW.
Je unadhani toleo la iPhone 6 ni kubwa sana? Apple wameleta kitu chochote kipya na cha kuvutia kwako kupitia simu hizi?
Kitu kingine kwenye Iphone 6 na 6+ = ni screen zake ANT-SCRATCH, sasa hutoitaji kuanagaika kununua screen protector kila mara..
Asante Denis kwa nyongeza hii!!! (y)