Wakati teknolojia hii ya ChatGPT kutoka kampuni ya OpenAI inakua kwa kasi kwa sasa wao Apple wameamua kabisa kuipiga marufuku kwa wafanya kazi wake.
KingIne ni kwamba Apple pia wamewakataza pia kutumia teknolijia zingine za AI (Artificial Intelligence)/akili bandia ukiachana na ChatGPT pengine mpaka kampuni itoe tamko.
Hii si mara ya kwanza kwa makampuni kuweka misingi fulani na kutoa makatazo ya kutumia huduma/bidhaa fulani ambazo zinatoka katika makampuni mengine.
Kuna fununu pia zinasema Apple imefikia uamuzi huo kwa sababu na yenyewe inakuja na teknolojia yake ambayo ina mfumo kama wa ChatGPT.
Kingine ni kwamba kampuni ina hofu kubwa kwamba inawezekana kama wafanyakazi wake watakua wanatumia ChatGPT basi inawezekana hata mfumo huo ukavujisha siri za kampuni hiyo.
Kumbuka Apple sio wa kwanza kupiga marufuku kwa wafanyakazi wake kutumia ChatGPT hata Samsung na wao walifanya hivyo baada ya mambo yao ya ndani kuvuja kwa kupitia huduma hiyo.
OpenAI pia wamekua wakapata baadhi ya kesi na shutuma kuwa huduma yake hiyo kwa namna moja au nyingine inavyjisha taarifa za watu/makampuni.
Kwa upande mwingine OpenAI kwa sasa iko katika maandalizi ya kuja na huduma ya ChatGPT ya kulipia kwa ajili ya biashara.
Kazi yake kubwa inakua ni kuwasaidia wale wa makampuni kuweza kuwa na uwezo wa ziada katika mamlaka ya kuongoza taarifa zao katika kampuni.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment. Je unadhani ni sawa kwa makampuni mengi kuipinga ChatGPT?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.