Apple ni wazi kwamba wana mambo mengi kwa sasa na moja wapo ni kuandaa Airpods Pro ambayo itakua ni kama msaada kwa watu wenye shida ya masikio.
Airpod Pro ni moja kati ya kifaa cha Apple ambacho kimefanya vizuri sana na vile vile kimeipatia mapato mengi katika kampuni ya Apple.
AirPods Pro hizo ni kwamba zitakua na uwezo wa kucheza sauti na midundo flani kwa mvaaji ili kugundua hali ya kiafya ya sikio la mtumiaji.
Kifaa hichi kinafanya kazi kama App ya Mimi ambayo tayari ipo na inafanya kazi kama Apple wanavyotaka AirPods Pro iwe.
Apple imesemekana kwamba walikutana na waandaaji wa App hiyo (Mimi) miaka kadhaa iliyopita, pengine hii ndio sababu ya Apple kufikia kutaka kutengeneza AirPods Pro ya aina hii.
Kingine kizuri ni kwamba Apple wana mpango pia wa kuifanya AirPod Pro hiyo kuweza kupima joto la mvaaji kwa kutumia tundu la sikio la mvaaji.
Mpaka sasa haiku wazi kwamba ni lini AirPod Pro za aina hii zitaanza kupatikana katika soko lakini kinachojulikana ni kwamba zitapatikana huku zikiwa na tundu la Type-C.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani AirPod ya aina hii ikitoka italiteka sana soko na kufanya vizuri kuliko zilizopita? Naindikie hapo chini katika uwanja wa maoni
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.