Apple mara kwa mara wamekua wakifanya mambo kadha wa kadha yakiwa ni kati ya marekebisho ya vitu ambavyo wanaona haviko sawa.
Mara kwa mara pia Apple, wamekua wakichukua maoni ya watu na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanaweka vitu vyake vizuri ili kuzidi kuwa juu zaidi.
Kumbuka kwa sasa iOS 71.2 toleo la majaribio (beta) imeshatoka tayari na pia hata TvOS 17.2 toleo la beta nayo imetoka na masasisho ya programu endeshi hizi zimekuja na mambo mapya.
Matoleo hayo yanaonyesha dhahiri kwamba hivi karibuni Apple itaunganisha moja kwa moja iTunes Movie Store Na App ya Apple TV.
Kwa sasa bado watu wanaweza kununua filamu (movie) au hata michezo ya kuigiza (Tv Shows) ukiwa ndani ya App ya TV.
Ukiachana na hayo yote bado pia watu wanaweza kupata filamu hizo na michezo hiyo kupitia katika App inayojitegemea inayojulikana kama iTunes Store App.
Kuna muda kama wewe ni mtumiaji mzuri wa vifaa vya iOS unaweza ukaona ujumbe ambao unasema “iTunes Movies moved to the Apple TV app.”
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unaipa hongera Apple kwa kufanya hili?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.