Makampuni mawaili makubwa duniani yanayojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa simu na teknolojia zingine mbalimbali yaliburuzana mahakamani takribani miaka minne (4) iliyopita. Kampuni la Apple lilikua likiamini kuwa baadhi ya ubunifu wake uliibwa (Chukuliwa bila ridhaa) na kampuni la Samsung na kuutumia katika simu zake.
Apple wameshinda kesi hiyo ambayo ni ya zamani kidogo na cha kushangaza kuhusu kesi hii ni kwamba hata simu zilizopigwa marufuku kuuzwa marekani (U.S) ni zile za matoleo ya zamani kidogo kutoka samsung.
Samsung inatakiwa kuacha kuuza baadhi ya simu zake ambazo kwa mtazamo mwingine ni kama zishatoka katika soko (hazina mapinduzi sana kwa sasa). Kesi hiyo ya muda mrefu imefungwa wiki hii na Mahakama ya wilaya ya kaskazini mwa California. Mahakama hiyo iliamuru kuwa baadhi ya simu za samsung ziacha kuuzwa kabisa kutoka katika kampuni la samsung — simu hizo ni za zamani kama mashtaka yenyewe — na kwa mtazamo mwingine zimeshaaga soko kabisa.
Simu Ambazo zimepigwa marufuku kuuzwa ni hizi zifuatazo
Samsung Admire
Galaxy Nexus
Galaxy Note
Galaxy Note II
Galaxy S II
Galaxy S II Epic 4G Touch
Galaxy S II Skyrocket
Galaxy S III
Stratosphere
Kama ulikua una mpango wa kujichukulia simu mpya moja kati ya hizi kutoka Marekani (US), inabidi ukae na utafakari tena. Ubunifu ambao Apple wanalalamika uliibwa na kampuni la Samsung ni pamoja na kile kipengele cha “slide to unlock”, kingine kikiwa cha kuotea meneno (predictive text) na kingine cha ‘Auto correct’.
Bila ya kujali upo upande gani katika swala (kesi) hili hakuna hata simu mpya yeyote kutoka samsung ambayo itakua imeshikiliwa bado na maamuzi haya. Matoleo yote mapya yako katika usalama.
Swali hapa linaweza tokea, kama kesi kama hii inaweza endeshwa kwa muda mrefu kiasi hichi mpaka bidhaa inatoka katika soko na kukaribia kupotea kabisa je, ni haki? — Mbona hukumu haikutolewa wakatik bidhaa ikiwa sokoni kabisa — kwa sasa hakumu ilivyotoka kampuni hilo la samsung halitapata hasara kwa kiasi kikubwa juu ya kutouza simu hizo ukilinganisha kama hukumu ingetoka katika kipindi ambacho simu hizo ndio zingekuwa sokoni kwa mara ya kwanza
Lakini ukifikiria kwa upande mwingine bado hukumu hii ina umuhimu wake na kwa namna moja au nyingine lazima itakuwa umeliumiza kampuni la samsung. Hukumu kama hii inaweza ikaua kabisa ubunifu,ushandani katika kampuni.
Kumbuka hukumu hii imetolewa marekani, usije ukashangaa maeneno mengine biashara zikawa zinaendelea kama kawaida. Hongera kwa kampuni la Apple kwa kuwashinda washindani wao juu ya kesi hii
No Comment! Be the first one.