Takwimu za mauzo ya simu janja kwa mwezi Julai pekee huko Uchina zinaonyesha kwa makampuni makubwa kama Apple kuzidiwa nguvu na washindani wenza.
Nchi ambayo Apple inapata wakati mgumu wa kufanikisha inaibuka kinara kimauzo ni Uchina; ni nadra kwa kampuni hiyo kuyazidi washindani wenza ambao ni wazawa nchini humo. Kwa mwezi Julai Honor imeweza kuwazidi Apple na Xiaomi kimauzo na kushika nafasi ya tatu.
Xiaomi imefanikiwa kuuza rununu 3.9 milioni, Apple (milioni 3) huku Honor iliuza simu janja 4 milioni. Nafasi ya pili walichukua Vivo kwa kuuza simu janja 5.3 huku kinara wao akiendelea kuwa Oppo na 5.6 milioni ya simu janja zilizouzika kwa mwezi Julai nchini Uchina.
Simu janja zilizozinduliwa/zenye 5G
Kwa mwezi Julai simu janja 26 pekee ndio ziliweza kuzinduliwa hii ikiwa ni pungufu ya 38.1% huku 11 tu zikiwa za 5G. Kwa ujumla kampuni zote ziliweza kuuza simu zenye teknolojia ya 5G karibu 29 milioni huku 23 milioni zikiwa ni za kisasa zaidi. Mauzo ya jumla ya simu janja yameongezeka kwa 28.6% huku yale ya 5G yakifikia 79.6%.
Mpaka sasa simu janja zenye teknolojia ya 5G zinafikia 400 milioni ambapo idadi hiyo inazidi watumiaji wa rununu Marekani na bara la Ulaya kwa pamoja.
Tumeendelea kukuhabarisha basi na wewe usiache kutufuatilia kila siku kwa habari zilizojikita zaidi kwenye ulimwengu wa teknolojia.
Vyanzo: China Daily, GSMArena
No Comment! Be the first one.