Baadhi ya simu janja-iPhone 12 na 12 Pro zimeingia kwenye mpango wa kurekebishwa na Apple wenyewe mara baada ya kuonekana kuwa na matatizo ya kiufundi hivyo kusababisha wakati mgumu kwa wanaozitumia.
iPhone 12 na 12 Pro zilizotengenezwa kati ya Oktoba 2020 na Aprili 2021 zimebainika kuwa na matatizo kwenye spika kiasi kwamba Apple wamekuanzisha programu ya kuzirekebisha bila ya malipo. Tatizo lenyewe ni mlio hausikiki wakati simu inaita lakini kwa mujibu wa nguli hao wanasema ni kiasi kidogo cha simu hizo ndio zenye tatizo hilo.

Je, wenye simu hizo wanatakiwa wafanyaje ili kuweza kupata huduma hiyo?
Kwanza maatengenezo hayo hayahusishi kabisa toleo nyinginezo kama iPhone 12 Mini au iPhone 12 Pro Max ambazo nazo zilizotoaka pamoja na hizo ambazo Apple imeanzisha programu ya kuzirekebisha.
Pili, Apple wenyewe wanafanya kazi hiyo lakini pia wana mawakala wake wanaowatatumbua/walioidhinishwa nchi mbalimbali duniani hivyo mtu akipeleka iPhone 12 au 12 Pro ambayo ina tatizo la kwenye spika basi itatengenezwa bila gharama yoyote ama kwa lugha rahisi huduma hiyo itakuwa ni BURE.
Wanaotumia simu hizo tajwa wanashauri kutunza data zao kwenye iCloud kabla ya kuipeleka simu janja kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo hayo ya kwenye spika. Habari ndio hiyo haya sasa kazi kwenu.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.