Kampuni ya Apple ambayo makao makuu yake yapo huku California Marekani imempoka mhandisi wa kampuni ya Tesla ili kuupa nguvu mradi wake ya kutengeneza gari la umeme. Apple inatengeneza gari lake la kwanza ambalo litatumia umeme, tetesi zinasema kwamba kampuni hii ya kimarekani inayo maabara nchini Ujerumani kwaajiri ya mradi huu.
Chriss Porritt ambaye alikuwa makamu wa raisi wa uhandisi wa magari huko Tesla ameripotiwa kujiunga na Apple kwa mujibu wa mtandao wa Electrek wa Ujerumani. Chriss ataenda kukutana na wataalamu wengine ambao tayari apple wamekwisha wakusanya.
Apple wamekuwa wasiri sana juu ya mradi wao huu wa gari lao la kwanza la umeme, inasemekana kwamba wapo wataalamu wengi katika sekta hii ya magari ambao wamenyakuliwa kutoka makampuni mengine makubwa.
Kabla ya kujiunga na Tesla Chriss alikwisha fanya kazi katika makampuni mengine makubwa kama vile Land Rover alikoanzia kazi na pia Aston Martin ambako alikuwa ni Mhandisi mkuu, Mhandisi huyu alipata elimu yake ya Mechanical Engineering katika chuo kikuu cha Hertfordshire.
Inasemekana kwamba Apple wanatengeneza gari lao la kwanza ambalo litatumia umeme, mradi huu ambao umekuwa wa muda mrefu unafanyikia huko Ujerumani katika maabara maalumu na tetesi ni kwamba Apple imekusanya wataalamu wapatao 20 ama 15 ambao wametoka katika makampuni ya magari.
Gari hili la Apple linatarajiwa kuuzwa mwaka 2019 ama mwaka 2020, tofauti na magari ya kisasa ya Google ambayo yanajiendesha hili litakuwa ni lakuendeshwa kama vile magari ya Tesla.
Ingawa kampuni hii ina maabara ya ubunifu Ujerumani lakini gari hili linatengenezwa na kujaribiwa katika maabara nchini Marekani katika mji wa California, inategemewa kwamba gari hili litatengenezwa nchini Austria na kampuni ya Magna Steyr. Mradi huu ulipata kibali mwaka 2015 kutoka kwa wakuu wa Apple lakini ulikuwa katika vitabu toka mwaka 2008 ila ulizuiwa kutokana na ukweli kwamba biashara ya Magari ilikuwa mbaya mwaka huo.
Vyanzo: Mtandao wa Telegraph pamoja na mitandao mingine.
One Comment
Comments are closed.