Simu za Nokia Asha ni moja ya simu maarufu na zilizouzika zaidi kutoka Nokia kwa miaka yake ya mwishoni kabla ya kampuni hiyo kununuliwa na Microsoft na zinaendelea kuuzika vizuri ata baada ya kuwa chini ya Microsoft. Kwenye mipangilio ya familia za simu kulingana na uwezo wake kuna simu za kawaida, alafu kuna simu zinazoitwa ‘featured phones’ kisha zinafuata simu-janja (smartphones).
Simu za Nokia Asha nyingi zinaingia kwenye familia a ‘featured phones’, hii ikimaanisha ni simu zenye uwezo wa kiwango cha kawaida hii ikiwa ni pamoja na uwezo wa kupokea apps mpya, kutumia intaneti pamoja na mambo mengine mengi kama vile kuwa na kamera. Tofauti yake kubwa na simu-janja ni pamoja na kuwa simu-janja zinauwezo mkubwa zaidi wa kupokea apps zenye ukubwa zaidi na ata kiutendaji kazi zinakuwa na vitu kama RAM, prosesa na diski-uhifadhi wa kiwango cha juu zaidi kulinganisha na ‘featured phones’.
Ingawa familia ya simu za Nokia Asha zinawekwa kwenye kundi la ‘feautured’ bado inauwezo mzuri kwa matumizi ya kila siku ya kawaida, na kupitia ushirikiano na watengenezaji wa apps kuna apps mbalimbali zimetengenezwa kwa ajili ya simu hizi ili angalia kukufanya kutosononeka utamu wanaoupata watumiaji wa simu zenye Android au zile za iPhone kwa wingi apps walionao. Na hapa leo tumekuletea baadhi ya apps muhimu zaidi kuwa nazo kwa matumizi ya kawaida ya kila siku;
WhatsApp S40
WhatsApp ni moja ya app muhimu kabisa siku hizi kwa ajili ya mawasiliano. Hii inakuwezesha kuchati na marafiki wa nchini na nje ya nchi kwa uraisi kabisa, unaweza ipata kwa kubofya hapa – http://store.ovi.com/content/172049
CNN
Je unapenda kujua kinachotokea ulimwenguni kila siku? Ni muhimu! Kupitia app ya CNN pata habari mbalimbali za ulimwenguni kupitia simu yako. Bofya kuipata – http://store.ovi.com/content/212837
Video HD
Je kuna video ya mwanamuziki mpya imetoka na upo mbali na kompyuta? App ya Video HD inakuwezesha kutazama video kutoka mtandao wa YouTube, tena kwa kiwango cha HD. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/161242
Editori PDF
Fungua na soma mafaili ya pdf kwa uraisi kwenye simu yako. Kwa mafaili makubwa sana app hii inaweza chukua muda kidogo kuyafungua ila mwish0 wa huo muda utaweza kuyasoma kwa uzuri tuu. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/363956
Opera Mini Web Browser
Ulimwengu wa simu za ‘featured’ ungekuwaje bila Opera Mini? Mgumu kweli kweli! Tokea enzi za miaka ile kabla simu janja hazijaenea na kuwa bei rahisi ni Opera Mini ndiyo ilikuwa inatusaidia kutumia mtandao, na inaendelea kubakia bora. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/46870
Sophie Cam
Je wewe unapenda kupiga picha? ”Viselfizi’ vya hapa na pale? Basi Sophie Cam itakufaa. Hii inakupa uwezo wa kubadilisha muonekano wa picha yako. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/212085
Wiki Encyclopedia
Kuelimika ni jambo zuri sana. Epuka kujikuta unaitaji kufahamu jambo flani kwa haraka alafu kuuliza kwa watu ni soo au upo peke yako, hapo ndio umuhimu wa app kama Encyclopedia unakuja. App hii inakusaidia kusaidia kufungua na kusoma mtandao maarufu wa WikiPedia kwa urahisi. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/202207
Viber
Viber ni app nyingine maarufu duniani kwenye masuala ya kuchati. Viber inasifika kwa kukuwezesha ata kupigiana simu za bure na mwenzako anyetumia app hiyo. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/565945
Pocket Light Free
Umeme umezimika alafu hauna tochi? Giza nene? App hii inabadilisha kioo chako cha simu cha LED kuwa tochi pale unaitaji mwanga wa zaidi kuona kwenye giza. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/289818
Yes, mwishoni kabisa ni Facebook…hii haitaji maelezo mengi sana…Tunaielewa, ipakue kutoka hapa – http://store.ovi.com/content/238066
Kwa leo ni hapo tuu, je kuna jambo unataka lifahamu? Tuwasiliane kupitia akaunti zetu za Facebook, Twitter, Instagram au Google+ (Bofya kwenye jina kuungana nasi)
No Comment! Be the first one.