Katika mitandao ya kijamii pale unapoongelea Apps za kutuma na kupokea picha pamoja na video kupitia mtandao huwezi kuziacha Instagram pamoja na SnapChat. Leo fahamu zingine pia zenye uwezo kama wa hizo mbili.
App hizi zinatusaidia sana hasa katika kujulisha ngudu, jamaa na marafiki (Followers) wetu kuwa siku zetu zinaendaje, bila App hizi kungekuwa na tatizo katika kufanya hilo labda kwa sababu tumezoea sana App hizi au hatuna/hatujui mbadala wake.
Lakini kumbuka kampuni yeyote ambayo iko juu lazima itakuwa inatolewa macho (itakuwa na watumiaji wengi) na pia mengi yatategemewa kutoka katika hiyo App. Kwa mfano kwa Instagram naweza kusema kuwa nategemea waanzishe huduma ya ‘live Streaming’ kuangalia tukio pale linapotokea. Wakifanya hivi watakua wamepiga hatua na kuwaacha wengi nyuma.
Pengine labda App nazoenda kukuonyesha sasa haziwezi kuziba pengo la akaunti zako za Instagram na Snapchat, ila si vibaya kuzifahamu….kwani uwezi jua ipi inaweza kuwa maarufu sana ndani ya kipindi kijacho.
TiZR
Hii inatamkwa kama Tiza, hii ni huduma ya kijamii yak u ‘stream’ inayopatikana katika hii App.Watumiaji wanaweza wakatuma post zao mbalimbali katika nyakati zao tofauti tofauti na kuzi’share’ na marafiki zao.
Video za kwenye TiZR zinakaa kwa muda wa dakika 20 tuu kabla hazijafutika kabisa. Lakini post hiyo inaweza kaa kwa sekunde 10 zaidi kwa kila ‘Like’ itakayopata. Kwa mfano kama itapata like 7 inamaanisha itakaa kwa muda wa sekunde 70 mara tuu baada ya zile dakika 20 kuisha
Hii inawafaa sana kwa wale ambao wanatumia/walishawahi kutumia Facebook Live, Vine na Snapchat.. Ishushe bure kupitia iOS.
Describe
Ni App ya picha ambapo mtumiaji anakua muelezeaji/Vlogger (mpigaji stori hasa hasa kwa kutumia video) ambapo atakuwa akielezea vitu ambavyo watumiaji wengine wanaviona katika picha flani.
Kwa haraka haraka hii inaonekana kama Instagram tuu lakini katika upande wa ‘Feeds’ (pale picha zinapoonekana) kuna kiboksi kidogo pembeni ya picha kikionyesha video ya mtumiaji akielezea picha hiyo.
Pia ni nzuri kwa wale ambao wanatumia/walishawahi kutumia Instagram na Snapchat.. Ishushe bure kupitia iOS.
Knoto
Hii ni App ya ku’share’ picha ambayo inatumia teknolojia ya kubaini sura (facial recognition) ambayo inawezesha kifaa chako kiweze kutuma picha automatiki kwa familia au hata marafiki ambao wapo katika picha hiyo.
App hii ni ya aina yake kwani kitu cha kwanza inachofanya ni kuwatambua watu katika picha uliyopiga.Hii inalifanya zoezi gumu kuwa rahisi hebu fikiria, kwa mfano App hii itarahisisha kutuma picha kwa watu ambao walikua katika pati na wakapiga picha nyingi kwa pamojaau hata mjumuiko/mkutano wa family. Kila mmoja atapata picha yake bila shaka sio?
Hii inawafaa sana kwa wale watumiaji ambao walitumiaga Facebook moments na pia inapatikana bure katika soko la iOS.
Yovo
App hii inawezesha marafiki wengi kushirikiana katika kutengeneza Stori moja kwa kutumia picha na hata video. Watumiaji wana uwezo wa kuandika au hata kuchora katika picha. Hili ni jambo zuri kwani linaleta furaha kwa watu ambao wanaweza ongezea kitu Fulani katika picha ili mradi picha hiyo iwe ya aina yake.
Yovo kwa haraka haraka inaonekana kama SnapChat tuu, lakini hii ya aina yake zaidi kwani marafiki zako wote wana uwezo wa kuongeza kitu katika post zako jinsi watakavyo wao.
Hii inawafaa sana kwa wale watumiaji ambao walitumiaga SnapChat na pia inapatikana bure katika soko la iOS and Android.
CyberDust
App ya meseji zenye usalama wa hali ya juu (hakuna mtu mwingine anaewea kusoma isipokuwa wewe tuu) ambayo inamuwezesha mtumiaji kutuma ujumbe,picha, linki na kadhalika. Vitu atakavyotuma vitapotea ndani ya sekunde 24 baada ya kusomwa. Ni mtandao wa kijamii ambao watumiaji wanaweza kukuza idadi yao ya marafiki kwa kutumia familia, marafiki zao, watoaji ripoti na hata watu maarufu na kuweza ku ‘share’ kilicho katika akili yao bila ya kuwa na uwoga wa kufuatiliwa.
Utumiaji wa App hii inaweza ukaonekana kama ni mgumu katika kipindi cha mwanzo sema kadri mtumiaji anavyozidi kutumia ndivyo anavyozidi kuielewa App hii.
Hii inawafaa sana kwa wale watumiaji ambao walitumiaga SnapChat na WhatsApp, pia inapatikana bure katika soko la iOS and Android.