Zamani wengi walikuwa na wasiwasi ya kwamba kuna kampuni moja tuu ndiyo inamiliki karibia ya kila huduma tunayotumia ya intaneti, nayo ni Google! Ila sasa zinakuwa mbili, haipingiki kabisa ya kwamba kwa sasa wengi wetu lazima tujekute tunatumia huduma za makampuni mawili zaidi. Nazo ni Google na Facebook!
Facebook pia wamejitaidi kuingia katika maisha yako kwa kiasi kikubwa! Unaweza kusema mimi nishajitoa Facebook, ila jiulize je utumii WhatsApp? Instagram? Naamini kwa haraka haraka zaidi ya asilimia 85 ya wanaomiliki simu janja (smartphones) na ata zile za kawaida kawaida lazima ziwe na WhatsApp…. hivyo lazima uwe katika familia ya Facebook.
Leo zifahamu apps zilizoshushwa zaidi 2014, na fahamu ya kuwa Facebook inamiliki apps zote za juu zaidi.
Namba 1 – Facebook Messenger – app inayokuwezesha kuchati na marafiki zako wa Facebook. Uwezo wa kuchati kutumia app ya Facebook uliondolewa mwaka jana.
Namba 2 – Facebook – app inayokuwezesha kutumia huduma za Facebook kwenye simu, zote ukitoa uwezo wa kuchati
Namba 3- WhatsApp Messenger – App inayokuwezesha kuchati na marafiki kwa kutumia intaneti, hii ikiwa ni pamoja na kutumiana mafaili mbalimbali kama vile picha, muziki n.k. Kampuni ya Facebook waliinunua WhatsApp kwa takribani dola bilioni 19 za Marekani.
Namba 4 – Instagram – App ya Mtandao wa kijamii unakuwezesha kupiga, kuzitengeza (badili muonekano) na kuweka picha kwenye akaunti yako na marafiki kuweza kuzipenda na kuzizungumzia. Instagram nayo ililinunuliwa na Facebook mwaka 2012.
Namba 5 – Skype – App ya huduma ya mawasiliano ya kupiga simu na kuchati ya Skype.
Namba 6 – Clean Master – App inayoisaidia simu yako hasa Android kufanya kazi kwa ubora zaidi. Inasaidia mambo kama utumiaji bora wa chaji na kupunguza vitu vinavyofanya simu yako iwe nzito sana. Tulishaielezea App hii, BOFYA HAPA KUSOMA -> Clean Master: Moja App Muhimu Kuwa Nayo
Namba 7 – Viber – Kama vile WhatsApp app hii inakusaidia kuweza kuchati na ndugu na marafiki kupitia huduma ya intaneti. Lakini zaidi ya WhatsApp, Viber inakuwezesha kupiga simu bure kupitia intaneti (kama Skype)
Namba 8 – LINE – Nayo inafanana na Viber zaidi, utaweza kuchati na kupiga simu.
Namba 9 – Twitter – Hii ni app ya mtandao maarufu wa kijamii wa Twitter. App hii inakuwezesha kutumia huduma zote za Twitter kama za mtandaoni kama vile kushiriki kwenye mazungumzo na pia kuweka tweets mpya.
Namba 10 – SnapChat – Hii ni moja ya app maarufu zaidi katika mabara ya Ulaya na Amerika lakini bado haijawa maarufu sana katika nchi yetu. SnapChat inakuwezesha kupiga picha, kuongeza mchoro au maneno kisha kumtumia rafiki yako aliye SnapChat pia. Akishafungua ujumbe (picha hiyo) ujumbe utajiharibu na kutoji’save’ kwenye kifaa chake.
Je unatumia apps gani zaidi kati ya hizi? Umegundua kitu kimoja hapo? Hakuna apps kutoka Google, na hii inaweza ikawa kwa sababu kwa watumiaji wa Android ambao ni wengi tayari simu zao zinakuja na apps nyingi za Google.
– Pia fahamu Apps zilizoshushwa zaidi kwenye simu za iOS (Apple) tuu kwa mwaka 2014, BOYFA HAPA!
Je unamaoni yeyote? Kumbuka tunapatikana kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram . Pia unaweza kutuandikia barua pepe teknokonatz (at) gmail dot com.
No Comment! Be the first one.