Ikiwa simu yako ya Android haina kasi, wala nafasi ya ziada ya kuongeza programu nyingine ni wakati sasa wa kufuta baadhi programu ili kuondoa matatizo hayo.
Baadhi ya programu za simu za mkononi hutumia kiwango kikubwa cha nafasi na kiwango kikubwa cha matumizi ya Betri na hivyo kuathiri utendaji wa simu yako.
Katika utafiti mpya wa simu za Android zaidi ya milioni tatu uliofanywa, watafiti wametaja orodha ya programu zinazokula sana chaja ya Betri kwa kiwango kikubwa na zile zinazochukua nafasi zaidi katika simu.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Kampuni ya usalama wa kimtandao ya Avast miongoni mwa programu zilizoongoza kwa ulaji wa Betri ni zile za Google wenyewe, kama Google Maps, Google Play Music, Google Plus na Google Hangouts.
Programu hizi huja pamoja na mfumo Endeshi wa Android na hata kama huzitumii hufanya kazi kwa nyuma ya mfumo pale tu simu inapokuwa umeiwasha zenyewe zinatumia data.

Aidha pia kuna programu/apps zingine zinazokula Betri kwa kasi ni zile za Samsung kama AllShare, ChatON na Push Service.
Vile vile watafiti hao wamegundua kwamba Google Docs na Text-to-Speech ni miongoni mwa programu zinazoongoza kula Chaji sambamba na Samsung WatchON, Video Editor na Media Hub.
Programu zingine zilizoorodheshwa kula Chaji ni SHAREit, Flipboard, Line na Adobe Acrobat Reader.

Wakati Avast wakitoa ripoti ya Programu zinazokula Chaji pia na zile zinazokula nafasi kubwa katika
simu yako hazikuachwa nyuma.
- Programu zilizoorodheshwa kwa kuongoza katika ulaji wa nafasi ni pamoja na WhatsApp, WeChat na Snapchat ambapo zimetajwa kuwa sambamba na zile za Netflix na Spotify.
- Instagram, Facebook Messenger na Snapchat zimetajwa kula nafasi kubwa sawa na Amazon kindle na BBC News App.
- Avast iligundua pia vivinjari (Browser) vya Chrome, Firefox na app ya barua pepe ya Microsoft Outlook pia zinakula Data kwa kiwango kikubwa.

Gagan Singh makamu wa Rais na Meneja mkuu wa biashara wa Avast amesema kwa maisha ya sasa simu janja zimekuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
Ushauri ambao umetolewa na Avast kwa watumiaji wa Simu za Android kwa wale ambao wanataka kuimarisha utendaji wa simu zao wasisite kuondoa (Kufuta) programu ambazo zinakula chaji ya Betri, nafasi hata kama wanazipenda.
Kampuni ya Avast imependekeza kuzuia Arifa (notifications), kuzuia Programu zinazofanya kazi zenyewe bila ya kufunguliwa.
One Comment
Comments are closed.