Asus ni kampuni ya kiteknolojia kutoka Tawain, kampuni inajihusisha na mambo mengi ikiwemo na kutengeneza na kuuza simu.
Simu zake ambazo ni toleo la Zenfone ndio zinakusadikika kwamba zitaachwa kabisa kutengenezwa huku wengi wakiwa wanahoji sababu zitakua ni zipi?
Kuna makampuni mengi ambayo yalikua yakitengeneza na kuuza simu lakini kwa sasa yameachana kabisa na biashara hiyo kwa mfano HTC na LG je na Asus anawafuata hao?
Kilicho washtua wengi ni pale kampuni ilipoamua kuwaachisha kazi wafanyakazi wote ambao wanatokea katika timu nzima ya Zenfone.
Simu hizi za Zenfone zilikua na sifa ya kuwa na umbo dogo lakini kuwa na sifa za undani ambazo ni za juu –kuliko vile unavyofikiri kwa kuzingalia kwa macho
Lakini cha kushangaza pia kwa simu hizi ni kwamba hazijawahi kuuzika kwa ukubwa huo (mauzo madogo) pengine ikawa ni hali ambayo imepelekea kitengo hicho kufungwa.
Kilichofanyika ni kwamba wafanyakazi wote katika timu za Zenfone wamehamishwa na kuwekwa katika vitengo vingine mbalimbali.
Hii inaonyesha kabisa kwamba huu ndio mwisho wa simu ambazo zinatoka chini ya kitengo hicho za Zenfone.
Lakini cha muhimu ni kwamba matoleo mengine ya simu kutoka katika kampuni hiyo ya Taiwan zitaendelea kutoka kama kawaida tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je hii umeichukuliaje? Je unadhani ni mapema sana kwa kampuni kufunga kitengo hicho?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.