Simu ya kamera siku hizi ndio mpango wa kwenda kidijitali zaidi na kuwa huru kupata picha zenye ubora kulinggana na uwezo wa kamera kwenye simu husika. Asus Zenfone 6 ni rununu ambayo ina utofauti wa aina yake, pengine kuja kuvutia wateja wengi.
Inaweza ikawa ngumu kidogo kuelewa maana ya “Kamera mbili kwa moja” kutokana na maana halisi iliyojificha ndani yake lakini kwenye ushindani unaokuwa kila leo ni lazima kuwa wa kitofauti kwa kile ambacho unataka kukipeleka kwa wateja ambao ni wengi na wenye kupenda vitu vizuri na si bora kitu. Haya yote utaweza kuelewa mara baada ya kupata kufahamu undani wa simu janja, Asus Zenfone 6:
Urefu wa kioo|Kipuri mama
Moja ya sifa kuwa simu janja fulani ni nzuri unachagizwa na toleo/aina ya kipuri mama ambacho kimewekwa humo ili kuifanya rununu husika kuwa na uwezo mkubwa wa kukamilisha kazi zake. Asus wameamua kutumia Snapdragon 855 kwenye simu husika. Kioo chake ni cha LCD ung’avu wa 1080p chenye urefu wa inchi 6.4.

Diski uhifadhi|RAM
Simu hii imeenda sambamba na matoleo tofauti tofauti ya mwaka 2019 kwani uwezo wake wa kuhifadhi vitu kwenye simu uko hivi: GB 6 za RAM kwa GB 64 memori ya ndani, GB 8 RAM kwa 256GB diski uhifadhi lakini pia ikiwa na nafasi ya kuweka memori ya ziada.
Kamera|Betri
Tunafahamu vyema kuwa matumizi ya kamera yanachangia kwa kiasi kikubwa kumaliza umeme kwenye simu janja ila unaweza usiwe na mawazo sana iwapo betri la kwenye rununu husika lina 5000mAh, nguvu ya kuchaji haraka kwa 18W. Kwenye kamera sasa ndio utakumbuka kwenye utangulizi wangu nimesema “Kamera mbili kwa moja” maana yake ni kwamba simu hiyo ina kamera mbili tu zenye MP 48+MP 13 lakini yenye uwezo wa kutumika upande wa nyuma na mbele. Ili kuweza kunielewa, tazama picha jongefu hapo chini.

Bei|Mengineyo
Simu hiyo inatumia Android 9 (Android Q itaongezwa hapo baadae), teknolojia ya kuchaji ni USB-C, usama wa kutumia alama ya kidole umewekwa kwa nyuma kama kawaida, Google Assistant ipo, NFC, Google Pay vipo, inatumia 4G, sehemu ya kuchomekea spika za masikioni ipo pia. Bei yake ni $557|zaidi ya Tsh. 1,281,100 kwa ughaibuni.
Simu hiyo upatikanaji wake kwa sasa ni kwa kuiagiza hivyo basi hatuna budi kuwa na subira kuisubiri ifike kwetu. Nini maoni yako kuhusu simu hiyo? Usiache kufuatilia TeknoKona kila leo!.
Vyanzo: Asus, 9to5Google
One Comment
Comments are closed.