Avatar za 3D sio kitu kigeni katika mitandao ya kijamii, na tunazitumia sana lakini katika mtandao wa WhatsApp hili halikuwepo hapo mwanzoni.
Ni wazi kwamba teknolojia hii –Avatar za 3D—ilianza kutumika mwaka 2019 katika mtandao wa Facebook lakini baada ya hapo Meta ikaamua kuisambaza kwenye huduma zake zingine na sasa imekuja katika WhatsApp.
Sasa ni zamu ya WhatsApp na uzuri wake ni kwamba ni wewe mwenyewe ambae unatengeneza Avatar hiyo kwa kuchagua aina ya nywele, mavazi n.k.
Dhumuni la hili ni katika kuhakikisha kuwa unaweza ukajitengenezea mdoli ambao unakaribia kufanana na wewe kwa kiasi kikubwa.
Ndani ya mtandao huu unaweza ukaliwezesha hili kwa kufanya haya.
- Angalia kwanza kuna sasisho (update) lolote kutoka WhatsApp na hakikisha unalipata.
- Ingia katika App ya mtandao huo na kasha nenda katika eneo la Settings.
- Gusa katika eneo la Avatar.
- Chagua “Create your Avatar” ili kuanza kutengeza Avatar yako
- Endelea kutengeneza taratibu mpaka umalize!
Mpaka hapo nategemea utakua umeshatengeneza mdoli ambao unafanana nao kwa kiasi kikubwa ambao utakua unautumia ndani ya mtandao wa huo.
Unaweza kutumia kama kuiweka Avatar hiyo kama sehemu ya picha katika ukurasa wako (Profile picture) lakini kingine ni kwamba utakuta zaidi ya stika 36 tofauti tofauti zitakua na muonekano unaendana kabisa na hiyo avatar ambayo umeitengeneza.
Kuna baadhi ya mitandao ya kijamii huwa inatoa huduma hii bure lakini ndani yake kunakuwa na vipengele viinavyouzwa kama vile aina Fulani ya mawazi (mfano yenye chapa kama ya Gucci n.k).
Ukilingalia jambo hili kwa jicho la tatu unaweza ukasema mtandao wa WhatsApp na wenyewe labda unaandaa mazingira ya kaunza kufanya biashara na watumiaji wa mtandao huu.
Kipengele hiki kwa sasa kinapatikana katika baadhi ya maeneo ambayo yamechaguliwa lakini baadae kitaanza kusambaa duniani kote kwa watumiaji wote wa WhatsApp.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je utaweza kutumia huduma hii katika mtandao wa WhatsApp?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.