Programu tumishi (App) ya AzamTV ambayo ilianza kupatikana kuanzia julai mosi mwaka 2017 katika duka la Play store na Apple Store imefanikiwa kupakuliwa zaidi ya mara milioni moja kwa kipindi cha miezi sita.
Ndani ya programu tumishi ya AzamTV inamuwezesha mtumiaji kuweza kupata chaneli za Azam ONE, Azam TWO, Sinema Zetu, ZBC 2, Azam Sports HD, Azam Sports2, Real Madrid TV na NTV Uganda kwa Tanzania pekee.

App ya AzamTV imeonesha mafanikio makubwa kwa muda mfupi tangu kuanza kupatikana ambapo kwa sasa kwa Tanzania inashika nafasi ya kwanza katika programu tumishi zinazopakuliwa kwa wingi na zinazozalishwa nchini Tanzania.