Habari ambazo hazijathibitishwa rasmi na kampuni ya Microsoft ila zimepatikana kupitia maneno ya mmoja wa wahusika mkuu katika utengenezaji programu endeshaji ya Windows 10 ni kwamba hakutakiwa na toleo la Windows 11! Windows 10 ndio mwisho, hakutakuwa na toleo la namba nyingine tena.
Je hili linamaanisha nini?
Baada ya kuja na uamuzi wa kuruhusu uwezo wa mtu yeyote anayetumia toleo la Windows 7 au 8 liwe ni rasmi au la wizi aweze kupata toleo la Windows 10 kupitia intaneti, yaani ‘kuupdate’, wengi tayari waliona uamuzi huu unaashiria mabadiliko makubwa ndani ya kampuni ya Microsoft kuhusiana na usambazaji wa programu endeshaji yao. Na inavyoonekana ni kweli mabadiliko makubwa yanakuja.
“Right now we’re releasing Windows 10, and because Windows 10 is the last version of Windows, we’re all still working on Windows 10.” – Jerry Nixon, ‘Developer’, Microsoft
“..Windows 10 ni toleo letu la mwisho la Windows…” alikaliliwa moja wa watetengenezaji wa toleo hilo la Windows linalokuja. Hivyo inaonekana utengenezaji mzima wa toleo la Windows 10 utaondoa pia ulazima wa kuleta matoleo mapya ya Windows kila wakati.
- Kwa jinsi walivyoitengeneza Windows 10 sasa wataweza kufanya maboresho na mabadiliko mbalimbali ya kimuonekano na kiubunifu bila kuathiri ubora wa programu endeshaji hiyo.
- Hii inamaanisha wataweza kutoa masasisho (updates) ndogo ndogo mara kwa mara bila kuathiri programu endeshaji hiyo na hivyo kuondoa ulazima wa kuwa na matoleo rasmi kila baada ya muda.
Kumbuka toleo la Windows 10 litaweza kutumika katika vifaa mbalimbali kama vile simu, tableti, mashine za ATM, kompyuta na vifaa vingine vya elektroniki bila tatizo lolote. Microsoft wanapigania kuwawezesha watengenezaji wa apps/programu kuweza kutengeneza apps kwa ajili ya vifaa mbalimbali kwa mkupuo mmoja.
Tunategemea toleo la Windows 10 kupatikana rasmi kuanzia mwishoni wa mwezi wa saba [Tarehe ya Kuja Windows 10 Yafahamika!]
No Comment! Be the first one.