Siku chache zilizopita tuliandika kuhusu ujio wa programu mpya ya huduma ya Google Drive itakayomuwezesha mtumiaji kuweza kufanya backup ya mafaili na mafolda mengi zaidi kwenye kompyuta yake. Sasa inapatikana rasmi.
Kwa sasa haifahamiki kama Google Drive tena bali ni Backup and Sync from Google.
Programu hii mpya ni mjumuhisho wa apps/programu za zamani za Google Drive na Google Photos, app hizo hazitapatikana tena bali kazi zake zimechukuliwa na hii mpya.

Programu ya Google Drive kwenye kompyuta kwa kipindi kirefu iliwezesha mtumiaji kuweza kuwa na nakala ya mafaili yake salama kabisa mtandaoni kama tuu yamewekwa kwenye folda la Google Drive.
Kuanzia sasa mtumiaji ataweza kuchagua kuchagua ata mafolda mengine mengi zaidi yaliyopo kwenye kompyuta yake ata kama ni ‘Desktop’ nzima, pia kingine ni kwamba programu hii mpya itaweza kufanya backup ya hadi memori kadi na USB Drive/Flash zinazochomekwa kwenye kompyuta husika.