Wiki zilizopita kampuni za mitandao Tanzania waliongeza gharama za kutumia intaneti. Kama unataka kuweka mambo ya bajeti safi, unaweza kutumia zana ambazo tayari zipo kwenye simu yako au kushusha programu za kusaidia kubana matumizi ya intaneti.
Windows/ Lumia
Kwenye simu ya Windows 8, inaripotiwa kuwa na zana iitwayo DataSense kubana matumizi ya intaneti ila upatikanaji wa hii zana unategemea na mtandao unaoutumia. Zaidi ya hiyo, hakuna app inayojulikana zaidi kutokana na masharti ya mfumo wa windows.

Android
Kwenye Android kuna mbinu mbili. Mbinu ya msingi kabisa ni kutumia zana iitwayo ‘Data Usage Manager ‘ utakayoipata ukiingia ‘settings -> Data Usage’.
Kwa kutumia Data Usage Manager unaweza:
– Kuchunguza matumizi yako kwa ujumla.
– Kutambua app gani zinatumia data zaidi ili uchukue hatua zaidi.
-Kuzuia intaneti kwa app usizotumia. (Hii inarefusha chaji pia).
– Kujiwekea notisi pale intaneti (bando) linapoelekea kuisha.
– Kuipangilia simu Kukata kabisa intaneti pale bando linapoelekea kuisha.

Njia ya hii ya kubana matumizi inahitaji kuifanya mara kwa mara na inafaa kama tabia yako ya kuwezesha intaneti inafanana kila siku. Kama ungependa chaguzo zaidi tumia app ya My Data Manager na Onavo Data Count ambazo teknokona inaziamini.
iOS
Kwa simu na ipad za Apple, njia ya msingi ni kuingia kwenye Settings > Cellular. Ingawa hautaweza kuweka kiwango cha mwisho au kupata notisi juu ya matumizi kama ilivyo kwenye Androidi, utaweza kuamua app ipi iweze kutumia intaneti kati ya zile ulizozipakia.
Unaweza kuzuia app kutumia intaneti kimya kimya kwa kuingia kwenye Settings->General > Background App Refresh.
Pia, unaweza ukaingia kwenye settings->Notifications na kupunguza matumizi ya intaneti kupitia notisi za app zako.
Kwa msaada zaidi, wasiliana nasi kupitia teknokonatz (at) gmail dot com au kupitia akaunti zetu za Twitter, Facebook na Instagram .
No Comment! Be the first one.