Katika vitu ambavyo mtu aliyeumia/kupata majeraha sehemu fulani ni kupona sehemu husika mapema iwezekanavyo na kuondokana na adha ya kupata maumivu, ni kitu cha kawaida kumuona mtu amejifunga bandage sehemu aliyoumia.
Umeshawahi kusikia kuhusu ‘Bandage janja?’. Basi kama hujawahi kuisikia au kama ulikuwa unatamani kitu kama hicho kiwepo ulimwenguni sasa tambua ya kuwa bandage janja ipo kwani timu ya watafiti kutoka vyuo vikuu vya MIT, Nebraska-Lincoln na Harvard Medical School wametengeneza bandage janja ambayo inasaidia jeraha/kidonda kupona haraka mara tatu zaidi ya banadage/plaster.
Yaliyomo kwenye bandage janja na jinsi inavyofanya kazi.
Tiba hii inayopatikana kwenye bandage janja ina nyaya nyembamba ndogo sana (fibers) ambapo kila waya una uwezo wa kuwekwa dawa tofauti na waya mwingine na hivyo kuifanya bandage hiyo kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa/majeraha mbalimbali ndani ya muda mfupi.
Ina kifaa maalum (micro-controller) ambacho kinaweza kuunganishwa na simu janja/wireless na kisha kutuma kiasi kidogo cha volti kwenye fiber iliyochaguliwa halafu inapitisha chaji kidogo na kupelekea kutoa mafuta (dawa) kwenda kwenye moja ya sehemu ya jeraha.
Bandage janja moja ina uwezo wa kuwekwa dawa mbalimbali zinazoweza kutibu kidonda/jeraha husika.
Bandage janja inafanya kazi kutokana na kiasi cha dawa ambacho unaruhusu kutoka kwenye zile nyanya; ukiruhusu chaji kubwa kwa wakati mmoja inamaana kasi ya kupaona kwa jeraha husika itaongezeka.
Ujio wa bandage hiyo umesifiwa ingawa imeeleza kuwakuna umuhimu wa bandage janaja kuwekewa kioo ili mtu anayeitumia kuweza kuona maendeleo ya jeraha lake (kuona kasi ya kidonda chake kinavyopona).
Mchoro wa bandage janja.
Mpaka sasa bandage janja inafanyiwa majaribio kwa wanyama kwanza na kisha itafanyiwa majaribio kwa binadamu kabla ya kuruhusiwa kutumika na kuanza kupatikana sehemu nyingi duniani.
Mpaka hivi sasa imeonyesha matokeo mazuri nainaweza kuanza kupatikana miaka michache ijayo. Umeipokeaje habari hii? Tuambie kwenye sehemu ya maoni.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|