Theluji ni changamoto kubwa kwa nchi ambazo zinapata majira ya baridi kali, barabara hufikia hata wakati zinafungwa kwa sababu ya theluji kujaa na kuzuia usafirishaji.
Gharama kubwa hutumiwa ili kupambana na theluji wakati wa majira ya baridi, mara nyingi theluji huondolewa kwa kutumia chumvi ama kemikali nyingine ambavyo vyote kwa pamoja vina madhara kwa barabara pamoja na mazingira.
Kuepuka madhara ambayo yanatokana na njia za kawaida kuondoa barafu basi watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Nebraska-Lincoln wamebuni aina ya barabara ya concrete ambayo itakuwa inapitisha umeme na hivyo kuruhusu theruji hiyo kuyeyushwa kwa umeme.

Njia hii itaruhusu concrete iweze kupitisha kiasi kidogo cha umeme (kisicho na madhara kwa binadamu) na kiwango hichi kitasaidia kuyeyusha barabara, Concrete hii inaundwa na mchanganyiko wa kawaida kwa asilimia 80 na zinazobaki ni chengachenga za vyuma pamoja na kaboni. Mchanganyiko huu pindi unapopewa nguvu ya umeme kutoka katika chanzo basi husababisha joto katika concrete ambayo itawezakutumika kuyeyusha barabara.
Ubunifu huu ambao ulifadhiliwa na mamlaka ya usafiri wa anga ya Marekani unategemewa kuisaidia sekta ya viwanja vya ndege kupunguza uhairishwaji wa safari za ndege wakati wa baridi kali.
No Comment! Be the first one.