Samsung inatuweka tayari na simu inayokunjika kutoka kwao ambapo tayari ulimwengu unafahamu machache kuhusu hicho ambacho kitaletwa kwenye ulinngo wa ushindani.
Samsung kama moja ya kampuni nguli inatazamiwa kurudisha teknolojia ambayo ilitoweka kwa miaka mingi lakini hivi sasa ikiwa na teknolojia kwa maana ya kwamba ni ulimwengu uliotawaliwa na simu janja.
Ambacho ulimwengu walikuwa hawajakijua ni simu hiyo itauzwa liasi gani? Kwa kweli kama una matarajio ya kuinunua itakapotoka basi inakubidi ujipange vilvyo kwani bei yake sio ndogo wala ya kubeza hata kidogo.
Imeelezwa kuwa simu hiyo itagharimu $1,700|Tsh. 3,310,000 na ikiaminika kuwa itaitwa “Galaxy F” ambayo itatoka pamoja na Galaxy X mwezi Machi mwaka 2019.
Vipi bei ya simu inayokunjika imekushtusha? Sisi kazi yetu ni kukuhabarisha, kushauri halafu uamuzi utafanya wewe mwenyewe kwa utashi wako.
Vyanzo: Engadget, The Verge