Bei za GB a.k.a gharama ya kupata kifurushi cha GB 1 cha intaneti nchini Tanzania inabakia kuwa moja ya gharama nafuu zaidi Afrika na ata Duniani pia.
Katika ripoti ya kimataifa ya tafiti ya wastani wa gharama ya GB 1, World Mobile Data Pricing 2021, inaonesha kwa wastani Tanzania ipo kwenye kundi la mataifa yenye gharama nafuu zaidi ya data huku GB 1 ikiweza kupatikana kwa wastani wa Tsh 1,739.25, huku taifa la bei nafuu zaidi nchini Afrika likiwa ni Sudan – ambapo GB 1 inaweza gharimu takribani Tsh 630.
- Kenya GB 1 ni takribani Tsh 5,217.75
- Rwanda GB1 ni takribani Tsh 2,898.75
Mabadiliko ya bei ya vifurushi iliyokuwa imefanyika miezi kadhaa nyuma kabla ya hatua za TCRA na serikali kufanyika yangepandisha sana gharama ya intaneti nchini na kutufanya tuwe kwenye kundi la bei ya juu.
Kupata uelewa mzuri angalia ramani hii kuelewa jinsi gharama za kupata GB 1 zilivyo katika mataifa mbalimbali. Rangi ya bluu iliyokolea inawakilisha bei ya chini ya Dola moja, kundi ambalo Tanzania ipo.
No Comment! Be the first one.