Kwa sasa Playstation 5 ndio toleo la juu tuu katika matoleo ya Playstation, tangia itoke imeonekana ikikubwa na baadhi ya changamoto na sasa bei imepandishwa katika baadhi ya masoko.
Unaweza ukajiuliza kwa nini kifaa hicho kilipotoka kilikua kinauzwa bei Fulani na sasa bei hiyo inaongezeka katika baadhi ya masoko,hapa ndio kitu kilichotokea kwa vifaa vya Playstation 5.
Masoko ambayo yameathirika kwa kiasi kikubwa sana ni yale masoko makubwa kabisa, hili limetoka kabisa katika kampuni mama ya PlayStation, Sony.
Kisa kikubwa ni mfumuko wa bei na sababu zingine za kiuchumi ndivyo ambavyo vimefanya bei za vifaa hivi kuongezeka.
Ongezeko la dola za kimarekani 30 hadi 80 limeonekana dhahiri katika masoko ya Ulaya, Marekani, china, Mexico, Australlia, Canada n.k
Kama unakumbuka kuna kipindi tuliandika kuwa Playstation 5 pia zilizalishwa chache kipindi Fulani na sababu kubwa ikiwa ni ukosekanaji wa malighafi –kwa wakati – Soma Zaidi >>HAPA<<
Soma kila kitu kuhusiana na PlayStation >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni kubwa kama hii kuweka bei tofauti na ile ya mwanzo katika baadhi ya masoko yake?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.