Ripoti ya Benki ya Dunia imebaini kwamba idadi kubwa ya watu duniani ina simu za mkononi kwa sasa.
Takwimu zilizotoka Jumanne zinaonyesha kuwa karibu 75% ya idadi ya watu duniani ina simu za mkononi na ni kiashiria si tu ya mawasiliano, lakini pia wa kuelekea na kukua kwa biashara inayochochewa na mawasiliano, Benki ya Dunia ilisema.
“Idadi ya watumiaji wa huduma za simu duniani kotei, zilizolipiwa kabla (pre-paid) na baada ya kulipwa (post-paid), imeongezeka kutoka chini ya bilioni moja mwaka 2000 hadi zaidi ya bilioni sita sasa, ambapo karibu bilioni tano katika nchi zinazoendelea,” Banki ya Dunia inasema.
Sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa ikitambuliwa kama chanzo muhimu cha mapato kwa serikali, hasa katika nchi zinazoendelea, na zimehimizwa kusaidia watu wengi zaidi kupata huduma hii kwani inasaidia kuongeza ukuaji wa uchumi.

No Comment! Be the first one.