Umoja wa Ulaya umetangaza kanuni mpya itakayotaka simu zote zinazouzwa katika eneo hilo ziwe na betri linaloweza kubalishwa kwa urahisi na mtumiaji simu ifikapo 2027. Hatua hii ni sehemu ya juhudi pana za kupunguza taka za elektroniki na kukuza uchumi endelevu zaidi.
Chini ya kanuni mpya, betri za simu janja lazima ziwe “zinazoweza kutolewa na kubadilishwa na mtumiaji wa mwisho” bila kutumia zana maalum.
Hii ina maana kwamba watumiaji wanapaswa kuwa na uwezo wa kubadilisha betri zao kwa urahisi bila kuwa na ulazima wa kupeleka simu zao kwa mafundi. Mteja anatakiwa aweze kubadilisha betri kwa kutumia kifaa cha kawaida kinachopatikana kwa urahisi au kupitia kifaa maalumu ambacho kinatakiwa kiambatanishwe kwenye ununuaji wa simu.
Kanuni pia inahitaji watengenezaji wa simu mahiri kukusanya na kutumia tena 50% ya lithiamu kutoka kwenye mabetri yaliyotumika ifikapo 2027, na 80% ifikapo 2031. Hii itasaidia kupunguza kiasi cha lithiamu kinachoishia dampo.
Kumbuka soko la Ulaya la vifaa vya elektroniki ni kubwa na sheria zake hulazimisha mabadiliko yanafika hadi nje ya mipaka ya bara hilo, mfano tayari sheria za simu zote kutumia USB C zimefanya toleo la mwaka huu la iPhone, iPhone 15 nalo kuja na aina hii ya chaja.
Uamuzi wa EU wa kudai betri zinazoweza kubadilishwa ni ushindi mkubwa kwa harakati ya haki ya mteja ya ukarabati. Kwa miaka mingi, watumiaji wamekuwa wakikasirishwa na uamuzi wa makampuni ya utengenezaji simu kutumia ubunifu uliofanya suala la kubadilisha betri kuwa gumu kwa watumiaji wa kawaida. Hii imefanya ata simu kupoteza thamani nyingi iwapo mteja ataipeleka kwa fundi kubadilishwa fundi. Hii imesababisha kukua kwa idadi ya taka za vifaa vya elektroniki, kwani watu wanaona ni bora kufanya uamuzi wa kununua simu mpya pale simu zao zikianza kupoteza ubora wa kukaa na cheti kutokana na uchovu wa betri.
Kanuni mpya itawapa wateja wa simu uhuru mkubwa wa kuweza kubadili betri la simu na hivyo kupunguza kiwango cha utengenezaji wa taka mpya za vifaa vya kielektroniki.
Faida za kanuni mpya ya EU:
- Simu zitatumika kwa muda mrefu zaidi. Hii itaokoa pesa kwa watumiaji na kupunguza taka za elektroniki.
- Itasaidia kudhibiti upandaji wa wastani wa bei za simu janja. Kwa kuwa wateja wengi wataweza kukaa na simu zao kwa muda mrefu zaidi, hii itaongeza ushindani wa bei kwa watengenezaji simu ili kuwavutia wateja katika kununua matoleo mapya.
Changamoto
Changamoto kubwa wabunifu wanayokutana nayo ni suala la kuweza kuweka urahisi katika ubadilishaji betri bila kuathiri teknolojia ya kuzuia maji maji kuingia kwenye simu hizo. Kwa sasa simu nyingi zinauwezo wa kuingia ata kwenye maji na bado zikatolewa muda huo huo na kuendelea kufanya kazi kama kawaida. Urahisi katika utoaji na uwekaji wa betri jipya unaweza sababisha ugumu katika kuwezesha ufanisi wa hali ya juu wa teknolojia hii.
Soma pia – Kwa nini huwezi kutoa betri kwa urahisi kwenye simu janja za kisasaÂ
Wewe una mtazamo gani juu ya suala hili? Je unadhani uwezo wa kubadili betri kwa urahisi litakuletea manufaa yeyote?
Vyanzo: itWorld
No Comment! Be the first one.