Katika dunia ya leo ni kitu cha kawaida mtu kuweza kununua kitu kupitia mtandao na akakipata baada ya muda mfupi lakini unafahamu ni lini mtindo huo ulianzishwa?
Karibu robo karne iliyopita kufanya biashara mtandaoni (kuuza/kununua kitu kwa njia ya intaneti) ilikuwa ni kitu haramu na kisichokubalika na mamlaka husika.
Historia inaeleza kuwa kati ya mwaka 1971 na 1972 wanafunzi wa chuo kikuu cha Stanford na wengine kutoka MIT walipanga kufanya biashara ya bangi kupitia ARPANET–hii ilikuwa mbinu ya mapema sana ya kufanya mawasiliano ambayo baadae ilileta TCP/IP. Lakini hii haikuwa biashara ya kwanza kufanyika mtandaoni bali yanachukuliwa kama maelewano tuu.
Agosti, 11 1994 ndio siku ambayo biashara ya kwanza mtandaoni ilifanyika kwa sababu Bw. Dan Kohn (alitengeneza tovuti iitwayo NetMarket) alishuhudia rafiki yake kutoka Philadelphia akiweza kununua CD ya muziki kwa $12.48 pamoja na gharama za kumfikia.
CD hiyo ilinunuliwa kupitia tovuti ya NetMarket na kutumia programu wezeshi kuweza kuficha namba za kadi ya akaunti yake ili hata N.S.A wakijaribu kufuatilia muamala umefanya na nani wasiweze kujua.
Ukuaji wa bishara ya mtandaoni: Makadirio ya mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao kuanzia mwaka 2014-2021.
Kununua/kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao ilikuwa ikifanyika kwa siri kubwa na ndio maana ule muamala uliofanyika Agosti, 11 1994 unafahamika kuwa wa kwanza kwa sababu ulifanikiwa; pesa iliweza kutumwa kutoka akaunti moja hadi nyingine.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|