Hakuna ubishi Microsoft ni moja ya kampuni kubwa zaidi za kutengeneza program kuwahi kutokea. Watu wengi wanafahamu zaidi juu ya bidhaa mbili kubwa kutoka kampuni hii, Microsoft Windows na Microsoft Office, kwapamoja zikijumuisha program zinazotumiwa zaidi ulimwenguni.
Licha ya program, kampuni hii pia imejikita kwenye utengenezaji wa vifaa, mfano Simu za Lumia (walinunua kutoka NOKIA) pamoja na mfululizo wa tablet za Surface kutoka Microsoft ambazo ni maarufu kwa watu wengi zaidi. Lakini, hizi si bidhaa pekee zinazotengenezwa na kampuni hii yenye zaidi ya miaka 40 sokoni.
Tunakuletea bidhaa 10 ambazo hazijulikani zaidi kama zinazalishwa na Microsoft.
- Router ya Wi-Fi
Kwa kipindi kifupi cha mwaka 2002 na 2004, Microsoft walitengeneza bidhaa ya Router ya Internet ambayo kwa kiasi kikubwa imekidhi haja za watumiaji wengi zaidi wa Internet duniani. Kifaa ichi, kiliacha kutengenezwa May 2004 kutokana na ushindani wa soko. Kilikuwa na uwezo wa kutumia USB na kusambaza WI-Fi kwa watumiaji tofauti.
- Simu za Mezani zisizotumia Waya
Kabla ya Lumia, Microsoft walikua kwenye soko la Simu, japo hazikuwa Simu janja. Kwa kipindi icho, miaka ya 1998 simu za mezani zisizotumia nyaya zilikuwa ndo dili katika ofisi za kampuni nyingi. Hazikuwa ana upekee wa kutokuwa na waya peke yake, bali pia zilikuwa na uwezo wa kutambua sauti (Mfano, ukisema ‘Call James’ inapiaga) na vitu vingine vingi vizuri. Hata hivyo, mpango huu wa simu uliisha, na Microsoft hawakutoa tena matoleo ya simu mpaka kufikia kutoa Lumia.
- Mfumo wa Spika za Kidigitali.
Kama Apple na Beats by Dre walivyoungana kuwapa ladha wapenzi wa muziki, Microsoft pia iliungana na kampuni ya Philips, kuwapa wateja wake mfumo wa Muziki bomba, walioupachika jina la ‘Digital Sound System 80’. Spika hizi zilitoka miaka ya 1998, zilikua ni za kwanza kabisa ambazo hazikulazimisha kompyuta iwe na kadi ya sauti ili kutoa sauti. Zilikuwa zinavutia zaidi kwa staili yake, huku zikileta mfumo wa kubonyeza labda + au – kuongeza au kupunguza sauti.
- Mashine ya Kusoma Alama za vidole (Fingerprint Scanner).
Kama kuna bidhaa zilikuja kabla ya wakti wake, ni ‘Fingerprint Readers’ za Microsoft. Zilitambulishwa mwaka 2004, zikifanya kazi pamoja na Windows XP na Vista kwa ajili ya kuongeza Usalama wa Windows. Japo mashine hizi hazitolewi tena, matoleo tofauti yameendelea kutolewa, yakiunganishwa na baadhi ya kompyuta huku yakifanya kazi vizuri hadi na Windows 8.1
- Surface Hub.
Wengi wanauita Surface Hub kama Ubao Mweupe unaofanya kazi na windows 10. Kihalisia, ni Kompyuta kubwa sana ya ‘touchscreen’, inayofungwa ukutani kwa ajili ya kufanya kazi za Msingi zinazofanywa na ubao pamoja na kompyuta kama vile kuandika notisi mbalimbali, matangazo, video za moja kwa moja za mikutano. Ziko za aina mbili, kuna yenye nchi 55 inayoonyesha video za 1080p, na kubwa zaidi yenye nchi 84, inayoonyesha video za 4K.
- Michezo ya Watoto
Microsoft waliwekeza katika ulimwengu wa michezo ya watoto iliyodumu kwa miaka mitatu kwa kushirikiana na watengenezaji wa ‘Teletubbies’, ‘Arthur’ na ‘Barney’. Uzalishaji wa michezo hii ilikuwa na mafanikio na ilikua inaweza kuchezwa kupitia TV pekee na si kompyuta. Midoli hiyo, ililenga kuwaelimisha watoto. Ilijumuisha maswali ya ndio au hapana na kupata majibu kutuka kwa watoto. Bado haijajulikana sababu hasa ya Microsoft kushindwa kuendeleza uzalishaji wake.
- LifeCam
Microsoft wamekuwa wakitengeneza ‘webcam’ hizi tangu 2006, lakini watengenezaji wengine kama vile Logitech, wamefanikiwa zaidi kwenye soko kuliko Microsoft. Toleo la sasa la Lifecam, linaloitwa Studio, lina sensa ya kamera ya 1080p, lensi ya 8MP pamoja na kinasa sauti madhubuti. Kampuni itaendelea kutoa bidhaa hizi, hasa kutokana na sapoti yake ya kinasa sura cha Windows 10.
- Padi za michezo ya video za SideWinder
Padi hizi zilitambulishwa mwaka 1995 kama sehemu ya mkakati wa Microsofk kuhamia kwenye michezo ya kompyuta. Ilidhamiriwa ifanye kazi na mfumo wa Windows pekee, lakini pia zinaweza kufanya kazi na mfumo wa Linux au IOS. Microsoft walisitisha uzalishaji wa bidhaa hizi, na kuelekeza nguvu zake zote kwenye michezo ya Xbox One.
- RoundTable
Hii ni kamera, iliyopewa jina maarufu ya Meza ya duara. Iliandaliwa na timu ya utafiti ya Microsoft mwaka 2007 kama suluhisho la kamera mikutano ya moja kwa moja, yenye uwezo wa kuchukua video za watu katika nyuzi 360,m ikiwa na kamera 5 na vioo kadhaa. Kwa kipindi icho, ilikuwa inagharibu zaidi ya TSh 5Milioni kuwa nayo, huku ikiwa na uwezo wa kufanya kazi na Office 2007.
- Simu za Zune
Zune zililetwa mwaka 2006 kama mpango wa kupambana uso kwa uso na Apple katika soko la vifaa vya mkononi. Laikini kutokana na uwezo mkubwa wa Apple na ushindani wa soko, mwaka 2011 walisitisha kutengeneza Zune kutokana na hali mbaya ya Soko. Sasa Zune wameiunganisha na Xbox One, na kuingia kwenye utengenezaji wa simu janja za Lumia
JE NI IPI IMEKUFARAHISHA ZAIDI KATIKA BIDHAA HIZI?
Chanzo cha Makala haya ni mtandao wa TimesofIndia.
One Comment