Uwanja mzima wa teknolojia una sura ya kipekee na inasemekana kuwa kila ipitapo miaka mitano basi teknolojia huwa inabadili kabisa – kwa kiasi kikubwa – mpaka kufanya ile iliyokuwa ikitumika kusahaulika.
Makampuni mengi yanajitahidi katika kuendana na mabadiliko hayo kwa kutoa huduma na kutengeneza bidhaa bora zaidi kupitika teknolojia mpya.
Hapa ndipo makampuni yanapoamua kuzalisha bidhaa Fulani kwa kuhisi kuwa labda watabadilisha teknolojia kwa ujumla na kushangaa kuwa bidhaa hiyo isifanye vizuri katika soko kama walivyo panga.
Leo tutaangalia bidhaa chache ambazo zinatoka katika makampuni makubwa kabisa kama vile Apple na Microsoft ambazo hazikufanya vizuri kabisa.
• Windows Millennium
Licha ya kuwa kampuni la Microsoft lilipata mafanikio makubwa kutokana na programu endeshaji zake za Windows 95 na Windows 98 kampuni liliamua kutoa programu endeshaji nyingine baada ya hizo ambayo haikufanya vizuri hata kidogo. Programu endeshaji hiyo ilikuwa ikijulikana kama Windows Millennium.
Lengo kubwa la kampuni kuitoa hii ni kwamba kampuni liliona inabidi itengeneze kitu (OS) ambayo pengine inaweza kuendana na watu (kizazi) wapya na wakisasa zaidi.
Windows Millennium (Windows ME) ilisababisha matatizo kwa watumiaji wa OS hiyo walipoanza kuitumia, walipoitumia na hata walipomaliza kuitumia. Kweli kabisa, ni kwamba OS nyingi zinafeli kufanya kazi pale ambapo prosesa yake inatumia umeme mwingi lakini ME ilifeli mwanzoni kabisa kwani ilikuwa ikisababisha mpaka watumiaji kuchukia
Microsoft baada ya kuliona hilo wakatoa tolea la Windows XP ambalo lilikuwa kama ni toleo ambalo lilikuja kifukia mashimo yote yaliyosababishwa na Windows ME. Windows XP ilijipatia sifa ya hali ya juu haswa baada ya kuwa inaendana na matakwa ya watumiaji wake.
• Apple Newton
Hivi ulishawahi kusikia kuhusu hii bidhaa? Kama hujawahi pengine ni kwa sababu haikufanya vizuri katika soko. Bidhaa hii ilitolea na Apple baada tuu ya Steve Jobs kuachana na kampuni hilo. Jambo hilo ambalo likafanya Apple kuongozwa na wakuu ambao kidogo hawakuwa vizuri katika swala zima la ubunifu.
Newton iliachiwa mara ya kwanza mwaka 1993. Lengo kubwa la kutengeneza hii bidhaa ni kwamba kwa ilitegemewa kuwa msaidizi mkubwa kwa mtu (Personal Assistant) ambayo ilikuwa una uwezo wa kutachi (Touch-Pad).
Cha kushangaza ni kwamba bidhaa hiyo ilikuwa sio rafiki kwa mtumiaji kabisa cha kwanza kabisa ni kwamba ilikuwa ni kubwa. Ilikuwa na inchi 4.5 X 7 na ilikuwa na uzito wa karibu ya paundi moja. Tatizo lingine lilikuwa ni kwamba betri lake halikuishi kwa muda mrefu. Kioo chake cha LCD hakikuwa na mfumo mzuri sana ambao ulisababisha matatizo katika kusoma. Baada ya muda kampuni ilishushwa chini kabisa na kuwa katika mstari wa kufilisika. Kampuni ilishushwa katika mstari huo kwa kuzalisha bidhaa kama Newton. Bidhaa hii ilifanya vibaya kiasi cha kwamba watu wakaanza kufundishwa kupitia stori yake.
• Internet Explorer
Kabla hujaanza kunibishia tulia kwanza nikuelezee (Haha!). Internet Explorer (IE) ilianzishwa na baada tuu ya kuanzishwa ikapata umaruufu mkubwa. Lakini umaarufu huu ulikuja baada ya kuwalazimisha watu kutumia IE.
Sasa vipi watu walilazimishwa kuitumia? Kumbuka pale unaponunua kompyuta yako mpya kitu cha kwanza kuweka ni programu endeshaji (OS) na kumbuka zile ambazo ni maarufu zinatokana na matoleo yale ya Windows. Ukiweka moja kati ya matoleo hayo lazima IE uikute ndani kama kivinjari. Kwa kipindi hicho wenngi hawakuwa na ujanja ujanja wa kuweza kutumia vivinjari mbadala kwa IE na wachache walioweza walikuwa wakitumia Mozila Firefox na wengine Opera.
Umekubali Sio? Sasa IE ilikuwa ni moja kati ya bidhaa mbaya kwani kadri ya teknolojia ilivyokuwa ikikuwa hasa katika swala zima la spidi ya intaneti IE haikuendana na mabadiliko hayo. Intaneti iliongezeka kasi lakini cha kushangaza ni kama IE ilikuwa inapunguza kasi. Kwa muda huo bado watu walikuwa wamefubwa macho wakidhani IE ndio kivinjari ambacho kina spidi kubwa lakini baada ya ujue wa Mozila Firefox na Chrome wamefumbuka!
Watu wengi waliona kuwa IE ni kivinjari ambacho bado kinatumia miundombinu ya miaka ya 90 (hata wewe unaweza ukasema hivyo) na hapa tukubaliane kwamba ilizidi kuwa na umaarufu wake kutokana na kwamba ilikuwa ikijitokeza katika matoleo yote ya programu endeshaji za Windows ukiachana na Windows 10 na kuendelea.
Kwa sasa Microsoft wana kivinjari kipya kinachojulikana kama Microsoft Edge ambacho kwa kiasi kikubwa kinaendana na wakati huu na pia kinaleta upinzani kwa vivinnjari vyenye majina makubwa kama vile Mozila Firefox na Chrome.
Kwa haraka haraka ni kwamba Windows Millennium (Windows ME) ndio iliyoizaa Windows Xp. Newtown ndio iliyoizaa au kusababisha kuzaliwa kwa iPad huku Internet Explorer ikizalisha au kusababisha kuzaliwa kwa Microsoft Edge. Baada ya makampuni hayo kujifunza kutokana na makosa!.
One Comment
Comments are closed.