Bing ni kama Google tuu kwa maana kwamba ni ‘Search Engine’ yaani ni sehemu ya matafuto katika mtandao.
Bing inamilikuwa na kampuni ya Microsoft na huwa kwa kiasi kikubwa inaonekana katika kivinjari cha Edge. Licha ya kwamba Google ndio ambao wanaongoza kutumika zaidi kwa matafuto ya mtandao bado Edge na yenyewe ina sehemu yake.
Bing mara kwa mara imekua ikifanya maboresho kadha wa kadha nah ii ni makusudi kabisa katika kuhakikisha kuwa inaongeza ushindani kwa wapinzani wake haswa Google.
Moja kati ya maboresho yaliyofanywa ni kuweka akili bandia katika huduma hiyo ambayo itasaidia moja kwa moja katika kujibu matafuto—huduma hii inajulikana kama chatbot AI.
Bing Chat moving today to 10 chats per session / 120 total per day.
Engineering making steady progress with quality of experience giving us confidence to expand the testing. Let us know how it's working for you!
— Yusuf Mehdi (@yusuf_i_mehdi) March 8, 2023
Kivinjari cha Edge na chenyewe kimezidi kujipatia watumiaji wengi ukilinganisha na ilivyokua zamani maana namba imeongezeka maradufu.
Mpaka sasa Bing ni moja kati ya njia kuu za kutafuta matafuto mbalimbali katika mtandao, na Microsoft ikiendelea kupamabana inaonekana dhahiri kabisa kwa huduma hiyo itakua juu zaidi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je kwa namba ya watumiaji milioni mia kwa siku na namba ambayo Google wanayo (zaidi ya bilioni moja) unadhani huduma hizi mbili zitkauja kufikiana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.