Binti wa miaka 12 huko Marekani (Colorado) anashikiliwa na polisi baada ya kujaribu kumuua mama yake mara mbili kwa sumu kisa iPhone. Binti huyo alimuwekea mama yake sumu ya ‘Bleach’ kisa mama yake kumpokonya iPhone yake siku chache kabla ya tukio hilo.
Ilikuwaje?
Mara ya kwanza mama huyo kugundua kinywaji chake cha aina ya ‘smoothie’ kunukia harufu ya ‘Bleach’ alipotezea kwa kuzani mtoto wake hakuosha vizuri kikombe alichompea kinywaji hicho.
Mara ya pili mama huyo akakutana na harufu ya bleach kwenye jagi la maji chumbani kwake pale alipotaka kunywa, hapo ndipo alipohisi kuna ualakini.
Bleach ni mchanganyiko wa sumu kali ambayo huwa inatumika katika kusafisha, kutoa rangi na kung’arisha zaidi vyombo na vitu vingine mbalimbali.
Mama huyo alitoa taarifa polisi alipokuwa anatibiwa hospitalini. Polisi wamesema baada ya kumkamata binti huyo na kumuhoji amekubali kuwa alikuwa anataka kumuua mama yake kama kisasi kwa kumpokonya simu yake ya iPhone. Binti huyo anashikiliwa katika gereza la watoto na inategemewa atafikishwa katika mahakama ya watoto kwa kosa la kujaribu kuua.

Wengi wamegawanyika katika jambo hili, wengine wakisema mama amefanya makosa kuwahusisha polisi na kwamba jambo hili lingemalizwa kimalezi zaidi. Pia wengine wanasema alifanya kosa kumpokonya kama alimnunulia yeye mwenyewe.
Je wewe unafikiri mama alikuwa sahihi kuripoti polisi? Tunakukumbusha, ukimpokonya mtoto simu yake, kuwa makini naye 🙂 wazungu wanasema ‘You Never Know!’, yaani ‘Uwezi Jua!’!
No Comment! Be the first one.