Kampuni ya RIM (Research In Motion) watengenezaji wa simu maarufu za Blackberry wamesema simu zao mpya zitakazokuwa zinatumia programu mpya ya uendeshaji ya Blackberry 10 zitazinduliwa mwakani mwezi wa kwanza.
Taarifa hii imetolewa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Thorsten Heins, Januari 10 RIM itatambulisha simu mbili zitaazokuwa zinatumia mfumo huo mpya wa Blackberry 10. Kumbuka simu hizi ndio tegemeo la kampui hii kutoka kati kipindi kigumu zaidi kwao kibiashara, kwani mauzo ya simu zao yameshuka sana kutokana na kupanda kwa umaarufu wa simu za iPhone na zile zinazotumia Android.
Kwa mtazamo wanu simu hizi za Blackberry 10 zinauwezo wa kifanya vizuri, ata mimi nimeshavutiwa nazo kupitia mifano ambayo washaionyesha.
Katika simu watakazozileta hapo mwakani moja itakuwa na kioo kikubwa na itakuwa ya kugusa tuu (touchscreen) wakati nyingine itakuwa ni ya kugusa ila pia itakuwa na ‘keys’ za QWERTY.
Hivyo kama ulikuwa na mpango wa kununua simu ya Blackberry vuta subira hadi hapo mwakani kwani kiumweli simu za Blackberry ambazo zipo sokoni kwa sasa zina uwezo mdogo kulinganisha na zile za iPhone na za Android. Mkurugenzi wa RIM ametoa uhakika kwamba simu hizi ni zaidi ya zote zilizopo sokoni kwa sasa, je ni kweli? Ngoja tuvute subira tutafahamu hapo mwakani.
No Comment! Be the first one.