Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya BlackBerry amesema bado wana imani katika biashara ya simu janja na tayari wapo njiani kuleta matoleo mapya mawili ya simu za BlackBerry zinazotumia Android.
Kuna kipindi kampuni ya BlackBerry ilikuwa ndio mfalme katika matoleo ya simu janja ila muda ulibadirika na wakachelewa kukubali mabadiliko na hivyo wakajikuta nje ya ushindani, huku Android na Apple kupitia iPhone wakishika usukani wa soko la simu janja.
Mkurugenzi mkuu, Bwana John Chen katika mahojiano na shirika la utangazaji la CNBC huko Marekani amesisitiza ya kwamba Blackberry bado wanaimani katika biashara ya simu na wana uhakika wa kutoa matoleo mengine ya simu hizo ata baada ya matoleo mawili mapya yaliyo njiani kutolewa.
Simu ya BlackBerry Priv iliyokuwa ya kwanza kuja na toleo la Android huku wakiamini simu hiyo itafufua biashara yao imefanya vizuri kiasi flani, ingawa bado ni nje ya mategemeo yao. Simu ya BlackBerry Priv imeuzika kwa kiasi cha takribani simu 600,000 huku lengo la BlackBerry lilikuwa kuuza zaidi ya simu milioni moja. Wengi waliona simu hiyo iliyokuwa na sifa bora za kiusalama ingeuzika zaidi kama bei yake ingekuwa nafuu kidogo.
Soma Uchambuzi wa BlackBerry Priv – BlackBerry Priv, Sifa zake, na bei yake!
Je ushawahi kutumia simu za BlackBerry? Je unafikiri kama watatoa matoleo ya simu zao za BlackBerry zenye bei nzuri kwako utanunua tena? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja wa habari za Teknolojia, TeknoKona.com
Chanzo: Digit.in