Siku kadhaa zilizopita kampuni ya TCL, watengenezaji wa simu za BlackBerry, wametambulisha rasmi simu mpya ya BlackBerry Motion.
Simu hii ya BlackBerry imeenda tofauti na kawaida kwa kuwa haijaja na eneo la keyboard zilizozoeleka, simu ni ya mfumo wa touch tu (mguso).
BlackBerry Motion inakuwa pia moja ya simu zenye betri la ujazo mkubwa, betri lake ni la mAh 4,000. Simu hii pia inakuwa simu ya kwanza kubeba jina la BlackBerry yenye uwezo wa kuhimili muda mrefu ndani ya maji bila madhara yeyote.
Simu ya BlackBerry Motion inaweza kuingizwa hadi futi 3.3 ndani ya maji kwa muda wa dakika 30 bila kupata tatizo lolote.
Sifa zingine kwa undani;
- Kioo/display ya ukubwa wa inchi 5.5 (Resolution 1080 x 1920 – FHD)
- Pia Display yake ina ubora wa juu dhidi ya ukwanguaji (Premium anti-scratch), hivyo unaweza weka simu pamoja na funguo bila shida.
- Prosesa ya Snapdragon 625 SoC pamoja na GB 4 ya RAM
- Teknolojia ya Quick Charge 3.0, hii ikimaanisha inaweza chaji hadi kufikia asilimia 50% ndani ya dakika 40
- Jumba la simu ni la aluminiamu na hivyo usihofu kuhusu kudumu kwa simu
- Inakuja na toleo la Android 7.1 Nougat ila kufikia 2018 itapata toleo la Android 8.0 Oreo.
- Kamera ya Megapixel 8 kwa selfi na kamera ya megapixel 12 kwa nyuma.
Nje ya hapo teknolojia nyingine mbalimbali zinazokuja na simu za kisasa kama vile WiFi, Bluetooth, eneo la earphone n.k zinapatikana pia.
Bei na upatikanaji wake?
Itaanza kupatikana mwezi huu katika Falme za Kiarabu na kisha kuanza kusambaa katika mataifa mengine. Bei yake ni kwenye dola 463 za Kimarekani ambazo ni takribani Tsh Milioni 1.1.