Mambo yakiendelea kuonekana yanamuelekeo mzuri kwa kampuni ya Blackberry watoa habari itakayowafurahisha wengi.
i: Simu ya Q5!
ii: BBM kwa Ajili ya Android na iOS!
Kwa kuanzia hapo baadae mwaka huu wataingiza sokoni simu ya Q5 ambayo ni ya bei rahisi lakini ikiwa imebeba sifa nzuri kuifanya kuvutia wapenzi wapya na wa zamani wa Blackberry, kiukweli kwa muonekano wake ata mimi naitaji moja. 🙂 . Wakati matoleo yote mapya ya simu za Blackberry zinazotumia mfumo mpya wa uendeshaji (OS) wa Blackberry 10 zimekuwa ni simu za gharama kupitia Q5 kampuni ya Blackberry inalenga wateja ambao wana bajeti ya kawaida. Simu itapatikana katika masoko ya Amerika ya Kusini, Ulaya, Nchi za Uarabuni, Asia na Afrika, haitauzwa bara la Amerika kaskazini.
Sifa:
RAM=GB 2
Ukubwa wa Uhifadhi=GB 8
Kamera ya Mbele=MegaPixels 2
Kamera ya Nyuma=MegaPixels 5
Kioocha LCD inchi 3.1.
BBM Kuja Kwenye Android na iOS (Apple)
Kingine kikubwa ni kuifanya BBM kujitegemea na kutokuwa kitu cha kupatikana katika BlackBerry pekee. Blackberry Messenger (BBM) itatolea matoleo kwa ajili ya simu za Android na iPhones na hivyo kuleta upinzani kwa app maarufu ya Whatsapp (Upo hapo?).
Kuhusu suala la bei na tarehe kamili ya kuingia sokoni kwa Blackberry Q5 endelea kutembelea Teknokona.
No Comment! Be the first one.