Shirika la ujenzi wa ndege, usafirishaji na teknolojia la nchini Canada, Bombardier limefikia uamuzi wa kupunguza wafanyakazi wake wapatao elfu tano.
Katika tangazo lilitolewa na shirika hilo limesema ndani ya miezi 12 hadi 18 ijayo watapunguza wafanyakazi elfu tano huku zaudu ya nusu wakifanya kazi kwenye shirika hilo nchini Canada.
Pia, shirika hilo limefikia uamuzi wa kuuza chapa yao ya ndege ‘Q series‘ kwa thamani ya $900 na chapa yao ya ‘Havilland‘ kwa thamani ya dola za Marekani milioni 300.

Shirika hilo lameanza kuchukua hatua za kulifanya shirika hilo lifikie uwezo wake wa juu kabisa wa mafanikio ambapo mapato ya hilo katika robo ya tatu ya mwaka huu kabla ya kodi ukilinganisha na ya mwaka uliopita kwa kipindi hiko yameongezeka kwa kiasi cha $267 milioni.
Shirika hilo limejipangia kwa mwaka 2019 kuongeza mapato yake kwa asilimia 10, hivyo kufikia dola za Marekani bilioni 18.