Jaji mmoja katika mahakama ya jimbo la Sergipe nchini Brazil ametoa hukumu ya kulazimisha mitandao ya simu ya nchini humo kuzuia huduma ya WhatsApp kwa muda wa masaa 72 kuanzia mchana wa tarehe 2 mwezi huu wa tano.
Jaji huyo anaitaka WhatsApp itoe data za mazungumzo yahusuyo wafanyabiashara wa madawa, data hizo zinatakiwa kupewa kwa polisi na huku WhatsApp wakisema hawana huwezo wa kutoa data hizo.
Mitandao ya simu ya nchini humo ilibidi kuzuia huduma za WhatsApp kwani kutokufanya hivyo kungewaweka katika adhabu ya faini ya takribani dola $180,000 kwa siku (takribani Tsh 293,000,000 | Kes 18,000,000).
Mara ya mwisho huduma za WhatsApp kufungia nchini humo kulisababisha ukuaji mkubwa wa utumiaji wa app ya Telegram ambayo ni mpinzani mkubwa tu wa WhatsApp na inaonekana uhamuzi huu utazidi kukuza utumiaji wa Telegram.
Hii si mara ya kwanza, takribani miezi mitano iliyopita ilishafungiwa – Soma – Brazil: WhatsApp Ilipofungiwa Kwa Muda, Telegram Ilipata Zaidi ya Watumiaji Milioni 1.5 Wapya