Kumekuwa na pingamizi kubwa dhidi ya tozo la kodi la umiliki wa laini ya simu. Kila mtu alikuwa anafurahia kushuka kwa gharama za matumizi ya simu kilichotokea ndani ya kipindi cha miezi sita iliyopita furaha hiyo ilizimwa ghafla kutokana na serikali kutaka kuongeza kodi kwenye sekta hii muhimu.
Akizungumza kwa simu jana Makamba alisema: “Sikubaliani na hili suala na kupita kwake ilikuwa ni kuzidiwa nguvu. Lakini najua haliwezi likatekelezeka ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.”
Alisema msimamo wa wizara yake katika suala hilo ni tofauti kwani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha gharama za mawasiliano zinapungua… “Wizara hatukubaliani na kodi hiyo. Nia yetu ni kupunguza gharama za kupiga simu kwa kuwa ni kitu kinachowezekana.“Nia yetu ni kushusha gharama iwe sifuri kabisa, kitu chochote kinachopandishwa bei sisi hatukubaliani nacho kwa kuwa ni kuwaumiza wananchi wetu hasa wa vijijini. Bidhaa ambayo inatakiwa kushuka ni mawasiliano hivyo lazima iwe hivyo.~Mwananchi
Na kwenye mitandao ya kijamii kama Twitter moto unaendelea wa kupinga suala hili
Yaliyoandikwa magazetini kuhusu mimi na #NoSimcardTax; SITAACHA. Naomba mchukue namba za mawaziri humu muungane nasi: http://t.co/Cx8WU3LsKw
— John John Mnyika (@jjmnyika) July 19, 2013
Today I dedicate this tweet to all who quietly and without asking for recognition have worked hard on #NoSimCardTax campaign #ChangeTanzania
— Maria Sarungi Tsehai (@MariaSTsehai) July 18, 2013
Watu 16 to 1000 for two days , you are tested http://t.co/lXtQEeAe6Y #NoSimCardTax KWA NINI TULIPE VAT, sh 1000, Internet 14.5%
— Change Tanzania (@ChangeTanzania) July 17, 2013
namba za Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa 0754/0684-765644. tuma msg kwa namba hizo kupinga hii kitu #NoSimCardTax kutunyonya masikini
— BongoClanTz.com (@BongoclanTz) July 19, 2013
@MariaSTsehai mimi nitaendelea kukataa hiyo kodi mpaka itapo futwa rasmi. #NoSimcardTax
— K W I R I N. (@iLashayo) July 19, 2013
No Comment! Be the first one.