Lenovo wanaionesha katika maonesho ya CES 2016 tablet yao mpya ambayo unaweza kuigeuza kuwa Laptop, Projector ama kamera ya 3D kutokana na mahitaji yako. Tablet hii imekuwa ndiyo moja ya habari zinazoongelewa zaidi katika siku ya kwanza ya maonesho haya ya kimataifa ya bidhaa za electronics.
ThinkPad x1 ni tablet mpya kutoka kwa lenovo ikiwa na kioo cha inchi 12 ikiendeshwa na processor mpya ya kutoka Intel inayoitwa core M7. Tablet hii imepata “kiki” jijini Vegas kwasababu inakuja na moduli ambazo zinaweza kuifanya tablet yako kuwa Laptop, projector ama camera ya 3D.
Moduli hizi ambazo zinauzwa tofauti na tablet kwa wale wanaohitaji zimetengenezwa kubeba kazi maalumu na hivyo mtumiaji atahitaji kuzichomeka katika tablet yake ili kuweza kupata matumizi ya moduli hiyo.

Moduli ya kwanza ni ile inayo ifanya tablet kuwa laptop, hii moduli inakuwa na uwezo wa betri wa zaidi ya masaa matano pia inakuja na port za USB na HDMI. Kwa kuwa tablet haina uwezo mkubwa wa betri pindi mtu anapotaka kuitumia kama laptop basi atahitaji kuwa na uwezo wa betri zaidi ya ule wa kawaida lakini pia port za USB na HDMI ni muhimu saana katika matumizi ya vifaa vingine kama flash na bila shaka hii ndiyo sababu kuu ya kuviweka.
Moduli ya pili ni ile ya inayoifanya tablet yako kuwa projector,moduli hii ina kifaa spesheli ambacho kinafanya kazi kama projector ila tu ni kwamba ni kidogo kwa umbo. Moduli hii ikipachikwa katika tablet basi unaweza kuitumia tablet yako kufanyia presentation yeyote bila shida.

Moduli ya tatu ni ile inayoipa tablet yako uwezo wa kamera ya 3D.Ni ukweli kwamba teknolojia ya 3D imekuwa kwa kasi kwa miaka ya karibuni, kumekuwa naongezeko la watengenezaji wa printer zenye uwezo wa kuchapisha vitu halisi kama vifaa vya mashine na hii imesababisha kuwepo na uhitaji wa kamera za 3D ambazo ndio hutumika kupiga picha za kutumiwa katika printer za 3D.
Huu ni mwanzo wa mabadiliko katika sekta ya teknolojia ya tablet pengine, tunategemea saana watengenezaji wengine waatakuja na tablet tofauti na hii ila pengine yenye mambo kama haya.
Kusoma habari zingine kuhusu teknolojia zinazotambulishwa katika maonesho ya CES yanayoendelea Las Vegas bofya hapa -> http://teknokona.com/tag/ces-2016/
No Comment! Be the first one.