App ya Facebook Messenger imekua na maboresho kadha wa kadha tangia ilipozinduliwa mwaka 2011. Kutoka katika kutuma na kupokea meseji na sauti za kawaida tuu mpaka kuwa na vipengele kadhaa
Hii inamaanisha kuwa kwa sasa Facebook Messenger haihusishi kutuma na kupokea ujumbe, sauti na picha tuu kwa mfano sasa watu wanaweza wakapata huduma ya kupiga simu ndani ya Messenger hiyo.
Kwa sasa mtandao huo maarufu zaidi, Facebook kupitia App yake ya Messenger imeamua kuonggeza kipengele katika App hiyo. Kuna gemu la siri ambalo linaweza likachezwa na marafiki.
Gemu hili linachezwa hivi: Mchezaji ataweza kecheza mchezo huu kwa kutupia mpira katika nyavu, kila atakaposhinda atapata chansi ya kwenda mbele zaidi. Kwa mfano atakapo ingiza mipira 10 kwenye nyavu ataweza kwenda katika sehemu nyingine (Level). Ili kufanya gemu kuwa gumu kadri mtu anavyoendelea kucheza, Goli litakuwa linatokea katika maeneo mbali mbali katika skrini.
Wachezaji pia wanaweza wakashindana ndani ya App hiyo ili kujua nani ameshinda sana katika kutupia mipira golini.
Hii sio mara ya kwanza kwa Facebook Messenger kuanzisha kamchezo Fulani kwa watumiaji wake. Hata mwaka jana walianzisha gemu ya Chess, ambayo inawezwa kuchezwa kwa kuandika @FBChess katika uwanja wa maongezi.
Kama unataka kupata michezo hii cha kwanza kabisa hakikisha unalo toleo jipya kabisa la Facebook Messenger.
Mitandao ya kijamii inakua sana siku hizi na mipya mingi inaanzishwa ili mtu kujihakikishia kuwa namba moja inabidi ubuni ufanyike. Ubunifu ambao utamfanya mtumiaji wa mtandao huo kuweza kubaki katika mtandao huo. Kwa mfano ukiingia katika mtandao wa TeknoKona una uhakika wa kupata habari mbalimbali za kiteknolojia kila siku (habari moto moto) sasa kwanini usibaki?