Simu za kawaida, maarufu kama ‘featured’ phones, ambazo huwa zinapatikana kwa bei nafuu zaidi ukilinganisha na simu janja (smartphones) zitaweza kuja na teknolojia ya 4G tena bila kuathiri bei zake.
Teknolojia ambayo ipo katka majaribio na maboresho kutoka kampuni ya Qualcomm itahakikisha chip hizo ndogo za mawasiliano ambazo kwa sasa zimekuwa zikitumika kwenye simu za bei za juu.
Chip hizi zikiwekwa kwenye simu katika hatua za matengenezo ya simu zitawezesha simu za kawaida tuu kuwa na uwezo wa mawasiliano ya 2G, 3G na 4G. Kwa sasa teknolojia ya 4G imekuwa kwenye simu ambazo kibei zipo juu kidogo.
Sifa kuu za chip hii
- Itawezesha simu za bei nafuu (entry-level/featured phones) kuwa na uwezo wa kuja na teknolojia ya 4G LTE.
- Uwezo wa hadi kasi ya kudownload ya Mbps 150 na kwenye mifumo ya 4G, 3G na 2G
- Inawezesha teknolojia ya 4G katika simu zinazotumia laini mbili kwa urahisi zaidi (Mitandao yote miwili)
- Utumiaji mdogo wa chaji na hivyo kusaidia simu hizi ambazo mara nyingi zinakuja na kiwango kidogo cha chaji kuweza kudumu katika intaneti ya 4G muda mrefu zaidi
Qualcomm wamesema tayari wameanza utengenezaji na uboreshwaji mkubwa wa chips hizo na wanategemea kuanza kuwauzia watengenezaji simu kati kati ya mwaka huu.