Ndio! Watafiti kutoka katika chuo kimoja huko marekani wamepata mafanikio makubwa katika majaribio yao ya kutengeneza chip za kompyuta kwa kutumia mbao.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa watafiti kufikia mafanikio kama haya na huenda itabadilisha kwa kiasi kikubwa mifumo ya vifaa vya mawasiliano tunayotumia kwa sasa.

Chip za kompyuta kwa sasa zinatengenezwa kwa kutumia silicon ambayo ni aina ya vitu vinavyo pitisha kiasi kidogo cha umeme, chips zilizo katika matumizi kwa sasa ni ngumu kuzitumia tena baada ya matumizi yake ya awali lakini pia haziwezi kuoza kwa haraka zinapotupwa na hivyo zilikua zinapigiwa kelele na wanaharakati wa mazingira.
Profesa Zhenqiang “Jack” Ma ambaye ndiye kiongozi wa watafiti hao anasema chip hiyo iliyotengenezwa kwa mbao ni rafiki wa mazingira kiasi kwamba ikitupwa msituni itaoza na kugeuka mbolea. Utafiti huo umechapishwa katika jarida la “Nature Communications”
No Comment! Be the first one.